Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema SMZ itaendeleza ushirikiano kati ya Zanzibar na Saudi Arabia ili kukuza uchumi wa nchi zote mbili.

Mhe. Hemed ametoa kauli hiyo alipofanya mazungumzo na Balozi wa Saudi Arabia Nchini Tanzania Sheikh Abdullah Alsheryan alipofika Ofisini kwake Vuga Jijini Zanzibar.

Amesema Nchi hizo zina uhusiano wa miaka mingi katika nyanja tofauti ambao unajenga ukaribu katika mashirikiano ya kujenga uchumi wao.

 

Mhe. Hemed ametumia fursa hiyo kumueleza Balozi huyo Fursa mbali mbali zilizopo nchini hasa katika uwekezaji na kumtaka Balozi huyo kuwaomba Wawekezaji kuja kuweza Zanzibar kwa kukuza Udugu wao.

 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amemueleza Balozi Abdullah kuwa Zanzibar ina fursa mbali mbali za Kitalii na kumtaka kuitangaza Zanzibar ili Wananchi kutoka Saudi Arabia kuja kujionea vivutio mbali mbali vya kitalii.

Amesema kwa kuwa Tamaduni za Nchi mbili hizo zinalingana na kumueleza Balozi huyo kuwa licha ya kuitangaza Zanzibar kiutalii bado Serikali inaendelea kulinda Mila na Tamaduni za Kizanzibari.

Kwa upande wake Balozi wa Saudi Arabia Nchini Tanzania Sheikh Abdullah Alsheryan amemuhakikisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuwa Saudi Arabia itaendelea kushirikiana na Zanzibar kwa Nyanja tofauti na kumuhakikishia kufanya mazungumzo na Wawekezaji kuja kuwekeza Zanzibar.


Abdulrahim khamis

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais

0 comments:

 
Top