Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema serikali ya Mapinduzi Zanzibar itaendeleza ushirikiano wake na Serikali ya Jamuhuri ya watu wa Kenya kupitia sekta mbalimbali ikiwemo masuala ya uwekezaji.

Mhe. Hemed ameleza hayo wakati akizungumza na viongozi wanaowakilisha wananchi kutoka Bunge la Kenya walipofika Afisini kwake Vuta kumtembelea.

Amesema serikali ya awamu ya nane imefungua milango yake kwa kuwakaribisha wawekezaji kuja Zanzibar kuekeza hivyo, amewataka viongozi hao kuitumia fursa hiyo kwa kuwaleza wananchi wa Kenya juu ya fursa zinazopatika Zanzibar.

Amefafanua kuwa, viongozi wakuu wa nchi kati ya Tanzania na Kenya tayari wameshaonesha nia njema ya ushirikiano mwema kwa raia wake huku akisisitiza hakutakuwa na vikwazo vyovyote kwa watakaokuja kuekeza Zanzibar.

Ameleza hivi sasa serikali ya mapinduzi Zanzibar imetilia mkazo katika uwekezaji kwa kukuza uchumi wake ambapo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ameanzisha Wizara maalum inayohusiana na uchumi wa Buluu.

Nae, Kiongozi msaidizi wa msafara wa wabunge kutoka Mhe. Musili Mawathe amemueleza Makamu wa Pili wa Rais faraja walionayo juu hatua ambazo Zanzibar inaendelea kuzichukua katika kupambana na maradhi Covid-19.

Akiwasilisha Salamu za spika wa Bunge la Kenya kiongozi huyo aliahidi kwamba serikali ya Jamuhuri ya watu wa Kuenya itaendeleza ushurikiano uliopo kati ya Kenya na Tanzania kupitia sekta ya mbali mbali ikiwemo Biashara na sekta nyenginezo.

Wabunge hao kutoka Kenya wakiambatana na wafanyakazi wa bunge hilo  wamekuwepo Zanzibar na wamepata fursa ya kutembelea maeneo mbali mbali ya utalii na sehemu za kihistoria pamoja na kushiriki katika michezo tofauti kwa upande wa timu ya wanawake na wanaume.


Kassim Abdi

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar. 

0 comments:

 
Top