Na,Jumbe Ismailly-MANYONI
KIKOSI cha Kuzuia Ujangili (KDU ) Kanda ya kati kimefanikiwa kuwakamata jumla ya majangili 128 kwenye mikoa ya Singida na Dodoma katika kipindi cha kuanzia mwaka 2016 hadi 2017 kutokana na makosa mbali mbali zikiwemo nyara za serikali.

Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia Ujangili Kanda ya Kati,Keneth Sanga alisema kuwa awali watuhumiwa hao walikutwa wakiwa na silaha,nyara za serikali,kuingia ndani ya mapori ya akiba ambayo yanapakana na mikoa hiyo iliyopo kanda ya kati. 

Aidha Sanga aliyataja mapori hayo ya akiba kuwa ni pamaoja na pori la akiba la Rungwa-Kizigo na Muhesi na kwamba katika kipindi hicho takwimu zinaonyesha kwamba hali ya ujangili inazidi kupungua. 

Hata hivyo Kamanda huyo wa KDU aliweka bayana kwamba jitihada zinazoendelea wanayaona mafanikio yanaonekana ambayo ni pamoja na kupungua kwa idadi ya watuhumiwa wanaowakamata. 

Kwa mujibu wa Sanga katika kipindi cha kuanzia mwaka 2016 hadi sasa 2017 jumla ya watu 6 wamepoteza maaisha yao kwa kuuawa na tembo katika mikoa ya Singida na Dodoma,mikoa ambayo ipo katika kanda hiyo,na kukitaja chanzo kikubwa cha watu hao kuuawa na tembo ni pamoja na kukosa kujua tabia za wanyama hao. 

“Manake mara nyingi unakuta wakiwaona wale huwasogelea na kutaka kupiganao picha,sasa yule ni mnyama hatari anataakiwa apewe umbali Fulani na unapomsogelea naye anadhani kuna hatari kwa hiyo katika kujilinda unakuta anamuumiza binadamu”alisisitiza. 

Ili kukabiliana na hali hiyo Kamanda huyo alisemaa wamekuwa wakitoa elimu kwa wananchi kufahamu kwamba siyo vyema kuanza kuwabughudhi wanyama hao kwani ni wa hatari. 

Katika hatua nyingine Kaimu Mkuu wa wilaya ya Manyoni,Miraji Mtaturu alirudia agizo lililowahi kutolewa na aliyekuwa Mkuu wa wilaya hiyo,Geofrey Mwambe dhidi ya wakazi 351 walioingia katika shamba la Tanganyika Pakers na wengine kuingizwa na viongozi wa vijiji bila kufuata taratibu za kisheria,kuwa wasiendelee kuongezeka tena

0 comments:

 
Top