Na Jumbe Ismailly-Iramba
DIWANI wa kata ya Ndulungu,tarafa ya Ndago,wilayani Iramba,Mkoani Singida amewaagiza mwenyekiti na afisa mtendaji wa Kijiji cha Kipuma pamoja na afisa misitu wa kata ya Ndulungu wanaotuhumiwa kuhusika katika uvunaji holela wa misitu ya miti aina ya mninga katika hifadhi ya msitu wa Kijiji hicho kuhakikisha wanakabidhi mbao 2,422 au fedha taslimu shilingi 24,220,000/= ifikapo feb,13,mwaka huu.

Diwani huyo,Iddi Mnyonga alitoa agizo hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la shule ya msingi Kipuma,kata ya Ndulungu,wilayani Iramba uliokuwa na lengo la kutekelezwa kwa agizo la mkutano uliopita ambao ulimwagiza afisa mtendaji wa kijiji hicho kutoa taarifa za mapato na matumizi ya kuanzia julai,2015 hadi dec,2015.

“Naomba nishauri hivi jumla ya miti aina ya mninga yote ni 346 ni miti mingi mno nah ii tumeitunza kwa muda mrefu,sasa naomba tuwape muda hii kamati ifanye kukamilisha,lakini naomba niagize kama diwani wa kata hii kama rais anatumbua majipu kule bandarini na hapa tutumbue nini,majipu”alisisitiza huku akishangiliwa na wananchi kwa kauli yake hiyo.

Aidha Mnyonga alifafanua kuwa kufuatia idadi ya miti hiyo 346 iliyokatwa kutakuwa na mbao 2,422,kwa hali hiyo watu wote waliotuhumiwa wahakikishe wanazirudisha mbao hizo kabla ya mkutano wa feb,13,mwaka huu na endapo hawatakuwa na mbao hizo watalazimika kukabidhi shilingi 24,220,000/= kinyume na kutekeleza agizo hilo hatua kali ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakani zitachukuliwa dhidi yao.

Kwa upande wao wenyeviti wa vitongoji wakithibitisha uharibifu huo wa ukataji miti aina ya mbao kihorela walielekeza tuhuma zao kwa afisa mtendaji wa Kijiji hicho,Godwini Gersoni,mwenyekiti wa Kijiji,Ramadhani Abdallah Salumu na afisa misitu wa kata ya Ndulungu,Helena Meliantoni kuwa ndiyo waliohusika kwa namna moja au nyingine miti ya mining kutoweka kwa kiasi kikubwa.

Iddi Selemani Hamisi ni mwenyekiti wa kitongoji cha Fundi majani alisema julai,21,mwaka jana yeye alichukuliwa na polisi na kuwekwa rumande kwa muda wa siku saba katika kituo cha polisi Sepuka na aliporudi alikuta miti hiyo imekatwa na alipowauliza wananchi walimwambia kuwa afisa mtendaji wa kijiji,mwenyekiti pamoja na afisa misitu wa kata ndiyo waliohusika kukata miti kwa madhumuni ya ujenzi wa shule ya kijiji chao.

Katika hali ya kushangaza mwenyekiti wa kitongoji cha Makungu,Omari Athumani aliweka wazi kuwa baada ya watuhumiwa wa ukataji huo wa miti walianza mazungumzo lakini walipofikia sehemu wakamtuma adukani kununua soda na aliporudi aliambiwa asiwe na shaka na wakati miti hao kwani wana haki zote za kisheria zinazowaruhusu kufanya uharibifu huo.

Hata hivyo katika utetezi wake afisa mtendaji huyo,….licha ya kukanusha kuhusika na uvunaji huo holela wa mining,lakini aliwataja baadhi ya viongozi na baadhi ya wananchi kuwa watu waliohusika kukata miti na kwamba endapo watakuwa wamemchoka ni bora wakatafuta njia nyingine ya kumwondoa badala ya kumsingizia jambo ambalo hajalifanya.

“Mimi ni kiongozi wenu na ninyi ni wananchi wangu labda kama kuna kile nilichokifanya ukaona siyo sahihi nilenge katika kilee,siyo unibebeshe mzigo ya miti hii yote kwa sababu kuna sheria kule mpo mnashabikia,lakini tutakapoingia kwa kina ule mti uliokatwa upo kwenye eneo lako na wewe utatakiwa kujibu pia”alibainisha afisa mtendaji huyo.

“Kwa Hatibu pale zipo mbao nay eye alikwenda kuchana kwa kutumia sensoo,sasa hebu niambieni hivi mtendaji huyu mmemchukia kabisa,muuweni basi afe kabisa asionekane…na mimi utakapoonekana wewe umebainika sijui nikufanyeje,lazima tuseme ule ukweli”alisema huku akionyesha kusikitishwa na taarifa hizo anazodai kuwa hazina ukweli wowote.

0 comments:

 
Top