Na,Jumbe Ismailly-Singida 
TUMBAKU ni zao pekee lenye madhara mengi ya kiafya kwa wakulima na wateja wake ambao nusu yao hupoteza maisha duniani kila baada ya sekunde nane,ambapo mtu hufariki kutokana na matumizi ya tumbaku.

Watu wanaotumia tumbaku katika umri mdogo vile vile hufariki mapema sana kabla ya kufikia umri wa miaka 25 na kwamba matumizi hayo ya tumbaku husababisha vifo milioni sita duniani kila mwaka.

Kwa mujibu wa taarifa za wataalamu wa magonjwa yatokanayo ya tumbaku nusu ya vifo vitokanavyo na uvutaji wa sigara ni kwa watu wenye umri wa kati ya miaka 30 hadi 69

Aidha uvutaji wa sigara duniani kote unachangia asilimia 12 ya vifo vyote katika nchi zinazoendelea,na kwamba wanaume ndiyo wanaokufa zaidi kutokana na uvutaji wa sigara.

Idadi kamili ya wavutaji wa sigara Tanzania haijulikani lakini ni ukweli usiopingika kwamba watu wanaoishi kwenye maeneo ya vijijini wanavuta zaidi kuliko waishio kwenye maeneo ya mijini.

ATHARI ZA TUMBAKU KIAFYA

Athari zinazotokana na matumizi hayo ya tumbaku kiafya ni pamoja na ugonjwa wa saratani ya mapafu na mdomo,magonjwa ya moyo,kiharusi,shinikizo la damu,kukosa mchumba au kuvunjika kwa ndoa,mwanamke mjamzito anayevuta hujifungua mtoto mfu au mwenye uzito pungufu (LBW<2 .5kg="" font="">

KEMIKALI ZA HATARI KWENYE MOSHI WA SIGARA

Moshi wa sigara una kemikali zaidi ya 4,000 na kati ya hizo,kemikali 60 huleta saratani,ambazo ni pamoja na saratani ya kemikali ya kuondoa rangi,sumu ya mchwa,Butane –gas inayotumika kwenye viberiti,kemikali iliyoko kwenye betri za magari,DDT –inayouwa wadudu kama vile mbu,Formaldehyde-inayohifadhia maiti. itaendelea  wiki ijayo.

0 comments:

 
Top