Na: Hassan Hamad (OMKR)
Maelfu ya waislamu kutoka maeneo mbali mbali kisiwani Pemba wakiongozwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, lao wamejumuika katika mazishi ya aliyekuwa Sheikh maarufu wa Ole Kanambe marehemu Sheikh Alawy bin Omar bin Salim Baalawy.

Sheikh Alawy ambaye amezikwa hapo hapo Ole Kanambe, alifariki jana usiku akiwa na umri wa miaka 81 baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Mmoja kati ya watoto wa marehemu sheikh Alawy, Sheikh Mussa bin Alawy amesema mbali na marehemu huyo kuwa na darsa kubwa kutoka maeneo jirani, wanadarsa wengine walikuwa wakitoka maeneo ya mbali kisiwani Pemba yakiwemo Tumbe, Fundo, Kengeja na Mkoani kufuatilia darsa zake.

Sheikh Alawy aliyezaliwa mwaka 1934 akiwa Sheikh maarufu katika eneo la Ole Kanambe kisiwani Pemba na Zanzibar kwa ujumla, ameacha kizuka mmoja na watoto 12.

Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahala Pema Peponi (Ammiin)

0 comments:

 
Top