Tamasha la Sauti za Busara litafanyika kuanzia tarehe 12 hadi 15 Februari mjini Zanzibar. Katika kipindi hicho wafanyakazi 150 wataajiriwa kwa ajili ya tamasha , asilimia 90 ni Watanzania, wote hulipwa mishahara na kuendeleza ujuzi wao mwaka baada ya mwaka. Sambamba na tamasha, Busara Promotions huhodhi mafunzo ya kiufundi na semina kwa wasanii, mameneja wa sanaa, wataalam wa vyombo vya habari, watengeneza filamu, mapromota wa muziki na wadau mbalimbali wa kiutamaduni. 

Dhima ya tamasha la mwaka huu ni ‘Together as One: Amani ndio Mpango Mzima’. “Kwa kupitia muziki wa moja kwa moja (Live) na filamu za Sauti za Busara, warsha na shughuli nyingine, tamasha huchukua nafasi pekee Zanzibar ya kuzuia unyanyasaji wa wageni, kulinda amani, umoja na heshima kwa utofauti kati ya watu.” Anasema Mkurugenzi wa Tamasha, Yusuf Mahmoud.

Sauti za Busara ni maarufu kwa wasanii wote kuimba ‘laivu kwa asilimia 100’. Wasanii wa ndani ambao wamezoea kuimba kwa mfumo wa playback katika maonesho yao hupata changamoto ya kuongeza uwezo wa maonyesho yao. Alikiba (TZ) na Rico Single (ZNZ) wote hawa hivi sasa wanajiandaa kufanya maonyesho ya kipekee kwa wahudhuriaji wa tamasha. Octopizzo, msanii mwenzao kutoka Kenya vivo hivyo amejipanga kutoa burudani ya kipekee na bendi yake katika tamasha hili la 12. 

Tanzania na Afrika Mashariki wanaweza kujivunia jukwaa hili ambapo wasanii wa ndani wanapata kuonesha kazi zenye kiwango katika steji la kimataifa pembeni ya wasanii wenzao wakubwa na maarufu kama Blitz the Ambassador kutoka Ghana/Marekani na Isabel Novella kutoka Mozambique ambao pia wanatarajiwa kudondosha burudani ndani ya Ngome Kongwe katika viunga vya Mji Mkongwe , Zanzibar. Wasanii wengine kutoka ndani ya nchi ambao wamejinoa kutoa burudani ni pamoja Msafiri Zawose, Leo Mkanyia, Ifa Band, Zee Town Sojaz, Mabantu Africa, Tunaweza Band na wengine wengi.

Ndani ya Afrika, fursa za kujenga ujuzi na mafunzo katika sekta ya ubunifu ni chache. Hivyo basi Sauti za Busara inahodhi mafunzo kwa vijana wa Afrika Mashariki, katika kuimarisha ujuzi na fursa kwa wenyeji ili kuweza kuunda mitandao na wageni ambao ni wataalam katika sanaa. Kama mshiriki mwenza wa African Music Development Programme (AMDP) mwaka huu tena mafunzo makubwa ya aina mbili yatashuhudia zaidi ya Watanzania 100 wakiboresha ujuzi wao katika Stage Management na Habari. 

Vile vile, Busara Promotions itahodhi vijana wa Kiafrika wenye utaalam katika tamasha na wanafunzi wa muziki kwa mafunzo ya miezi 2 pamoja na timu ya waandaaji wa tamasha; wanafunzi kutoka Ujerumani watakuja katika tamasha kwa ajili ya kujifunza pia. AMDP inaongozwa na International Music Council na kutekelezwa kwa ushirikiano na matamasha, mashirika ya muziki, vyuo vikuu na asasi zisizo za kiserikali nchini Cameroon, Congo, Côte d’Ivoire, Kenya, Malawi, Msumbiji, Tanzania, Uganda and Zimbabwe. 

Mkakati huu una dhumuni la kuisaidi sekta ya muziki Afrika kwa kupitia mfululizo wa utekelezaji mipango huku ukiwa na lengo ya kuongeza fursa za ajira. Programu inanufaishwa na msaada wa Umoja wa Ulaya pamoja na ACP Group of States.

Sababu kuu ya Sauti za Busara kuwa na mafanikio ni mabadilishano ya uzoefu kati ya wenyeji na wageni. Wenyeji wana ujasiri zaidi katika utamaduni wao na ukweli kwamba ni wa kipekee kwasababu wageni hutoka kila pande ya dunia kuja kuushuhudia. Wageni wa Kimataifa wanafahamu kwamba wanapata uzoefu wa kitu halisi na tofauti huku wakiburudika na Muziki wa Kiafrika bega kwa began na watu wa Afrika Mashariki.

0 comments:

 
Top