Idadi kubwa ya wananchi waliohudhuria tamasha la wazi la ‘Shtuka Sasa’ lililoandaliwa na kampuni ya simu za mikononi ya Zantel mwishoni mwa wiki hii wameipongeza kampuni hiyo kwa kuwaletea burudani hiyo visiwani hapa.
 
Tamasha hilo lililofanyika katika Uwanja wa Kiembe Samaki lilihudhuriwa na maelfu ya wakazi wa kisiwani humo ambao waliimba na kucheza na wasanii hao, liliandaliwa ili kuwapa fursa wateja wa Zantel kujifunza zaidi kuhusu huduma za kampuni hiyo.

Likitumbuizwa na wasanii wakali wa muziki wa kizazi kipya kama Chege, Madee, Dogo Asley, tamasha la Shtuka Sasa, lilifanikiwa kukonga nyonyo za wakazi wa Zanzibar kwa kiasi kikubwa.
 
Akizungumza wakati wa tamasha hilo, Afsa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan alisema tamasha hilo ni mfululizo wa mengine yatakayofanyika nchi nzima ili kuwapa fursa wateja wao kuzitambua zaidi huduma za Zantel na kuzifurahia.
 
‘Toka mwaka huu uanze, Zantel imejikita kwenye kuwaelimisha wateja kuhusu ubora wa huduma zetu kupitia matamasha, ambayo yatafanyika nchi nzima’ alisema Khan.
 
Tamasha la Zanzibar lilifunguliwa na wasanii wa kikundi cha B-Six wakifuatiwa na msanii Sultan King ambaye ni mmoja wa wasanii wanotamba sana kisiwani Zanzibar kwa sasa.
 
Wasanii wengine waliopokewa kwa shangwe kubwa ni Dogo Aslay na bendi yake ya Mkubwa na Wanawe ambao waliimba nyimbo zao kali kama ‘Mapenzi ya Kitoto’ na nyingine nyingi.
 
Baadhi ya wananchi waliohudhuria tamasha hilo wameipongeza kampuni ya Zantel kwa kuwaandalia burudani hiyo kisiwani hapo.
 
‘Kama kampuni inayoongoza kisiwani hapa tunaishukuru Zantel kwa kutuletea burudani nzuri ambayo pia imetupa fursa ya kujifunza zaidi kuhusiana na huduma zinazotolewa na kampuni yetu kama Mpaka Basi na nyinginezo’ alisema Ashfa Mohamed, mmoja ya mashabiki waliohudhuria tamasha hilo.
 
Pia ikiwa ni mwendelezo wa kampeni yake kuhamasisha wateja wao kusajili laini za simu, Zantel pia ilitumia tamasha hilo kusajili laini za wateja wao kupitia mabanda yaliyosambazwa uwanja mzima.

0 comments:

 
Top