Jumla ya shilingi Milioni 14,400,000/- zimetumika katika ununuzi wa vifaa mbali mbali vya michezo kwa ajili ya Timu za Soka zipatazo ishirini na Tatu za Jimbo la Kitope ndani ya Wilaya ya Kaskazini B.
Vifaa hivyo vimetolewa na Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi katika hafla fupi iliyofanyika kwenye uwanja wa Mpira wa miguu wa Timu ya Soka ya Kombora iliyopo Kitope na kuzishirikisha Timu zote husika.
Hafla hiyo ya vifaa vya michezo ikiwemo Seti za jezi na mipira kwa kila timu ilikwenda sambamba na Balozi Seif kukabidhi Track Suits kwa ajili ya Waamuzi wa Wilaya ya Kaskazini B pamoja na mchango wa Shilingi 3,000,000/- kusaidia uendelezaji wa ujenzi wa Jengo la Klabu ya Timu ya Soka ya Kombora.
Timu zilizowafanikiwa kupata msaada huo ni pamoja na Kazole United, Mgambo Combain, Kombora, Nundu Boys, Timu ya Skuli ya Kitope, Fujani Star, Mbuyuni Star pamoja na Small Villa.
Nyengine ni Kitope United, Villa Coast, Kitope Kids, Simba Watatu, Kinduni City, African Coast, Old Star, Fujoni Boys, African Boys, Cairo United, New Star, Mgambo Star, Bati, Blue Dinamol pamoja na Kichungwani.
Akizungumza na Wanamichezo hao Mbunge wa Kitope ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliwapongeza wanasoka wa Timu ya Kombora kwa uamuzi wao wa kujenga Jengo la kudumu la Klabu yao.
Katika kuunga mkono juhudi hizo Balozi Seif aliahidi kusaidia nguvu za kufikia hatua za linta na baadaye kufikiria hatua za ukamilishaji wake ili kuwaondoshea usumbufu wa makazi wanamichezo hao.
Balozi Seif pia alihidi kuwapatia Magoli ya chuma wanamichezo hao wa Timu ya Kombora ili uwanja wao uende na wakati kama vilivyo viwanja vyengine vya michezo hapa Nchini.
Mapema katika Taarifa yao iliyosomwa na Mmoja kati ya Viongozi wa Timu hiyo Khamis Khamis alisema wameamua kuendeleza michezo kulingana na Historia ya Vugu vugu la Nchi hii iliyotokana na sekta hiyo.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
0 comments:
Post a Comment