Jumla ya vikundi 32 kutoka ndani na nje ya nchi vimechaguliwa kufanya maonyesho ya muziki katika tamasha la 11 la Sauti za Busara ambalo limepangwa kufanyika kuanzia tarehe 13 mpaka 16 Februari 2014 katika viwanja vya kihistoria Ngome Kongwe, zanzibar.

Orodha ya wasanii imejumuisha imejumuisha wasanii maarufu kutoka Africa Mashariki, Kusini na Afrika Magharibi, pamoja na wasanii kutoka nchi za Mto Nile na hata maeneo ya Puerto Rico

Sauti za Busara (Sound of Wisdom) linalojulikana kama ‘Tamasha rafiki katika Sayari’ ni tamasha la kimataifa linalosheherekea muziki wa kiafrika kila mwaka wiki ya pili ya mwezi wa Februari. Lengo likiwa ni kuwaleta watu pamoja na kuonyesha utajiri wa muziki wa kisasa ambao umebuniwa katika nchi za Afrika Mashariki, nchi nyingine kutoka barani Afrika na kwingineko duniani.

Wasanii watakaopanda jukwaani kutoka hapa nyumbani ni pamoja na
Jhikoman nguri wa muziki wa Rege anayesifika hapa nchini na ambae ameshafanya maonyesho mbalimbali ya muziki ndani na nje ya nchi, ambapo kwa upande wa Sauti za Busara hii ni mara yake ya nne kupanda jukwaani. Jhikoman mpaka hivi sasa amesha toa albam tatu zinazojulikana kama Chikondi aliyoitoa mwaka 2005, Tupendane, 2008 na Yapo, iliyoingia sokoni mwaka 2009.

Taarifa za wasanii Sauti za Busara 2014

JHIKOMAN-Tanzania

Jhikoman ni mwanamuziki pekee bora wa rege nchini Tanzania, nyimbo zake hupendwa na watu wa rika tofauti na huzipiga kwa kingereza na Kiswahili tangu mwaka 1994. Ujumbe wa Jhikoman kwa jamii ni kusisitiza uelewa wa haki, amani, umoja na upendo. Jhikoman ameshatoa albamu kadhaa na kufanya maonyesho mbalimbali ndani na nje ya Nchi kama tamasha la Mela, jijini Oslo nchini Norway, World Village Festival mjini Helsinki, nchini Finland,
Exeter Respect Festival nchini Uingereza na Tanzania Tamasha la Sauti za Busara na ZIFF yote ya Zanzibar.

Mwaka 2005 alitoa albamu yake aliyoipa jina la “Chikonda” katika albamu hii aliutambulisha ubunifu wake kwa mashabiki wake wa Rege, albamu hiyo alishirikiana na wasanii mbalimbali wa kimataifa kama Baran M, kutoka Kurdistan, Khalid Salih, kutoka Sudan, Uriel Seri, kutoka Ivory Coast, Thorbjørn Holte, Geir Inge Storli, Henrik Johnsen and “Jacob” kutoka Norway, OnRebel G kutoka Mexico na Sister Yana kutoka Brazil.

Mwaka 2008 alitoa albam nyingine aliyoipa jina la“Tupendane” kutoka Red Studio ya nchini Finland. Na mwaka 2009 alishirikiana na Lebo ya Udumood Music ya mjini Helsinki, nchini Finland na kutoa albamu yake “Yapo” aliendelea kutoa ujumbe na maonyesho yenye kuvutia. Jhikoman anasema si kuinua mguu wako bali tumia akili na roho ikuongoze vizuri. Maneno ya Jhikoman hubeba ujumbe wa nguvu zaidi ya risasi. Safari ya muziki inandelea bila ya mipaka katika kushirikiana na wanamuziki wa kimataifa.

EBO TAYLOR- Ghana
Mpiga Gitaa, mtunzi, kiongozi wa Bendi na muandaaji wa muziki. Huyu si mwingine bali ni Ebo Taylor mzaliwa wa Ghana katika mwaka 1936. Ni miongoni mwa majina makongwe kwa miongo kadhaa katika tasnia ya muziki nchini Ghana. Mwaka 1962 alipeleka kundi lake la Black Star Highlife Band kwenda Uingereza ambapo walipata nafasi ya kufanya onyesho na Fela Kuti na baadhi ya wasanii wa Kiafrika.

Alivyorudi Ghana alifanya kazi kama Muandaaji wa muziki na kuandaa miradi yakembalimbali, sambamba na kuunganisha nyimbo za utamaduni za Ghana na kuchanganya vionjo mbalimbali vya muziki na kutengeneza aina yake ya mdundo katika miaka ya 70.

Mwaka 2010 Kazi ya Taylor imepata umaarufu yaani katika karne hii ya 21 kama muandaaji wa Hip-hop ambapo alitoa nafasi kubwa ya kutolewa kwa albamu yake ya kwanza iliyosambazwa kimataifa ya “Love and Death” kupitia studio ya Strut Records. Mafanikio yake yalifanya rekodi ya Strut kutengeneza stori ya Maisha ya “Highlife & Afrobeat Classics” kati ya mwaka 1973-1980.

SEVEN SURVIVOR - Tanzania

Seven Survivor ni kikundi kimoja wapo ambacho kinaongoza katika muziki wa mchiriku ndani ya jiji la Dar es Salaam. Aina hii ya muziki ambayo ni maarufu sana katika mji wa Dar es Salaam, mkoa wa pwani na Morogoro. Mchiriku imepigiwa kwa zaidi ya miaka ishirini sasa hasa kwenye sehemu ya watu wenye kipato cha chini.

Mwaka 2012 walishiriki tamasha la Sauti za Busara wakishindana na Jagwa Music in a Mchikichu washindani wao. Wana albam mbili, “Panya wa Dar es Salaam” (Rats of Dar es Salaam), walioitoa mwaka 2007 na 2013 walitoa albam ya “Kilio cha Mastaa” (weeping of stars), ikiwani kumbukumbu ya kumkumbuka kiongozi wao (Juma Mpogo) na wasanii wengine walioiaga dunia.

Seven Survivor Wanatunga nyimbo mbalimbali zenye historia ya matukio ya kila siku yanayozunguka jamii zao na nchi kwa ujumla. Nyimbo zao nyingi zinaelezea kuhusu matukio ya wizi, madawa ya kulevya, umalaya, ushirikina, ufanyishwaji wa kazi kwa watoto wa chini ya umri wa miaka 18 na migogogro tofauti

SONA JOBARTEH- Gambia
Sona Jobarteh ni msichana wa kwanza kupiga Kora na vifaa mbalimbali vya muziki, Kuimba, kutunga nyimbo kutoka katika familia ya Griot. Alizaliwa mwaka 1983 nchini Gambia (Afrika ya Magharibi).

Sona ametokea katika familia ya wanamuziki, Mjukuu wa Amadu Bansang Jobarteh, binamu wa mpiga Kora maarufu Toumani Diabate na vile vile dada wa Tunde Jegede. Alianza kujifunza kupiga kora tangu alipokuwa na umri wa miaka mitatu na kufanya onyesho lake la kwanza akiwa na umri wa miaka minne katika mkahawa wa London Jazz Café.
 
Pia amejifunza mambo mbalimbali katika chuo cha muziki cha “Royal College” ikiwemo Piano na harpsichord na baadae amekwenda chuo cha Purcell kwa ajili ya kujifunza utunzi wa muziki. Katika kipindi hicho alijihusisha na miradi kadhaa ya kimuziki kama “River of Sound” akishirikiana na Irish Chamber Orchestral na kufanya maonyesho ya pamoja na Royal Philharmonic Orchestra, Britten Sinfonia, Milton Keynes City Orchestra na Viva Chamber Orchestra.

Mbali na hayo ameshikiriana na wasanii kutoka sehemu mbalibmali duniani, ni mmoja kati ya wanachama wa African Classical Music Ensemble ambayo imeshawahi kufanya ziara za kimuziki sehemu mbalimbali duniani ikiwemo Uingereza, Ireland, Visiwa vya Karibian na Afrika. Jobarteh hutumia muda wake kufanya maonyesho na kutoa elimu ya upigaji wa Kora kwa ajili ya kuendelea utamaduni wa upigaji wa Kora kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Orodha ya wasanii Sauti za Busara 2014
Wasanii kutoka Afrika Mashariki
Jhikoman (Tanzania) Ashimba (Tanzania / Finland) Swahili Vibes (Zanzibar) Baladna Taarab (Zanzibar) Hoko Roro (Tanzania) Tausi Women's Taarab (Zanzibar) Joel Sebunjo ft. Lenna Kuurmaa (Uganda) Seven Survivor (Tanzania) Abantu Mandingo (Tanzania) Segere Original (Tanzania) Moyize (Rwanda) Ricky na Marafiki (Kenya) Rajab Suleiman & Kithara ft. Derya Takkali (Zanzibar / Turkey / Germany) Kazimoto (Tanzania / Germany)

Wasanii kutoka Bara la Africa na kwingineko duniani
Ebo Taylor (Ghana / Germany) Jupiter & Okwess International (DRC) Joe Driscoll and Sekou Kouyate (USA / Guinea) The Nile Project (Nile Basin) Noumoucounda Cissoko (Senegal) Oy (Ghana / Switzerland) Addis Acoustic Project (Ethiopia) Sona Jobarteh (Gambia / UK) Tarabband (Egypt / Sweden / Majestad Negra (Puerto Rico) HAJAmadagascar and The Groovy People ft. Werner Puntigam (Madagascar / France / Austria) Tritonik (Mauritius) Kara Sylla Ka (Senegal / Switzerland) Dizu Plaatjies & The Ibuyambo Ensemble (South Africa) Street Rat and Body Mind & Soul (Malawi) Moyize (Rwanda) Ricky na Marafiki (Kenya) Waldemar Bastos (Angola / Portugal) na wengineo wengi

 Wadhamini na wafadhili wa Sauti za Busara 2014: The Royal Norwegian Embassy, Hivos, Goethe Institut, the Embassy of the United States of America, Swiss Agency for Development and Cooperation, African Music Festivals Network, Zanzibar Unique, Memories of Zanzibar, Ultimate Security, the Embassy of France, Southern Sun Hotel, Azam Marine, the Embassy of Germany, SMOLE II, pamoja na ufadhili wa  vyombo vya Habari 2014, kama vile Times Radio FM, RFI-Kiswahili, and Hits FM Radio & Zanzibar Cable Television

0 comments:

 
Top