Chama cha Kisukari Tanzania (Tanzania Diabetic Association) kitakuwa na uzinduzi wa gari maalum la huduma za upimaji wa afya kwa magonjwa yasioambukizwa hususan kisukari (diabetes mellitus) na shinikizo la damu (high blood pressure) Gari hilo maalum lina vifaa vya maabara. Uzinduzi huo utafanyika tarehe 24.04. 2013 kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mhe. Dr. Hussein Ali Mwinyi (Mb) atazindua gari hilo. Tunawaalika wazee wanawake na wanaume ndio watakaopewa fursa hiyo ya kipekee kupima afya zao bila malipo sukari na presha. Uandikishaji una anza Saa 2 asubuhi hadi Saa 5. Huu ni uzinduzi tu gari hilo maalum litatumika kwa kazi hiyo katika sehemu mbali mbali nchini kutokana na ratiba itakayopangwa. Wajulisheni wazee watakaoweza kufika siku hiyo ya Jumatano 24.04.2013.
Taarifa hii imeletwa kwenu na Chama cha Kisukari Tanzania
Dr. Ali Mzige
k.n.y Tanzania Diabetic Association

0 comments:

 
Top