Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amesema kilimo cha kisasa kinaweza kuwakomboa wakulima kwa kuongeza uzalishaji na kukuza kipato chao.

Maalim Seif ameeleza hayo huko Makunduchi wakati wa ziara yake ya kutembelea kilimo cha kisasa cha Migomba ambacho kinatumia teknolojia mpya ya umwagiliaji.

Amesema iwapo kilimo hicho kitaendelezwa, kitaweza kuwakomboa wakulima kwa kuongeza tija na kupata maendeleo kwa kipindi kifupi.

Amewataka viongozi wa Mkoa wa Kusini Unguja kuwaunga mkono wataalamu wa kilimo hicho, ili waweze kuwaelimisha wakulima wengi zaidi katika eneo hilo na mikoa mengine ya Zanzibar.

Kwa upande wake mkulima wa kilimo hicho bw. Haji Kinazi amesema tayari ameshaona mafanikio ya kilimo hicho na kwamba anakusudia kukiendeleza zaidi ili aweze kujikomboa kiuchumi.

Amesema tatizo kubwa lililokuwa likimkabili ni uhaba wa maji, lakini hivi sasa wanaimarisha miundombinu ya maji na kuendeleza kilimo hicho kwa uhakika.

Nae mtaalamu wa kilimo hicho bw. Omar Mohd amesema mazao yatokanayo na kilimo hicho cha kisasa ni mazuri na yanaweza kuleta tija kubwa kwa wakulima.

Amesema kupitia utaalamu huo migomba inaweza kustahamili maradhi na ukame, na kuwawezesha wakulima kupata mazao mengi yaliyo bora ambayo wanaweza kusafirisha nje ya nchi.



Hassan Hamad, OMKR.

0 comments:

 
Top