Busara Promotion ilianzishwa kama NGO ya kitamaduni 2013 hapa Zanzibar. Tukio kubwa linalofanywa kila mwaka ni tamasha la Sauti za Busara. Ni tamasha maarufu linalowaleta watu pamoja katika kusherehekea muziki wa Afrika Mashariki na kwengineko.

Tarehe 9th Novemba, Busara Promotions iliitisha mkutano na waandishi wa habari Zanzibar juu ya suala la muimbaji hodari wa nyimbo za utamaduni Fatma Baraka anayejulikana kwa jina la Bi Kidude. Mkutano huo wa waandishi wa habari uliitishwa kwa ajili ya kutoa taarifa za akiba za fedha za Bi Kidude kwa wanafamilia wake kisheria. 

Mkutano huo wa waandishi wa habari ulifunguliwa kwa wawakilishi kutoka Busara Promotions, kuyajibu madai yasio na ushahidi yaliotolewa na wanafamilia wa Bi Kidude yanayoshutumu kuwa Busara inamtumia vibaya Bi Kidude. Kwa bahati mbaya mwanafamilia huyo huyo alikataa kuhudhuria mkutano and pia alipinga kutoa ruhusa ya Bi Kidude kuwepo mkutanoni.

Mkutano ulihudhuriwa na waandishi wa habari 30, wawakilishi kutoka wizara ya utamaduni, wanafamilia wengine wa Bi Kidude na marafiki wengine. Kwa sababu isiyojulikana, habari zilitangazwa kwenye vyombo vya habari kuwa Busara Promotions inaachana na kumtupa Bi Kidude. 

Busara Promotions imeendelea kumsaidia Bi Kidude tangu kabla ya mwaka 2005. Miaka saba iliopita, Busara Promotion imemtangaza Bi Kidude na kutambuliwa na WOMEX (World Music Expo), Bi Kidude alipata tunzo kubwa katika maisha yake na kuchangiwa fedha ili kuendeleza muziki wake wa kiutamaduni. Tunzo ya WOMEX ilikuja na kiasi cha yuro 5,000. Baada ya hapo kama ilivyopendekezwa na WOMEX, Busara Promotions ilimsaidia katika kuzitunza na kuzitumia fedha zake katika kutengeneza paa na sakafu ya nyumba yake iliopo Raha Leo Mjini Zanzibar, pamoja na kuitia Plasta, kutengeneza mabomba ya maji, kuikarabati na kuipamba vyema. Bi Kidude mwenyewe alikuwa akichukua kiasi kisichopungua 50,000 Tsh kila wiki kwa muda wa miaka saba. 

Katika nafasi nyingi Busara Promotion imemsaidia Bi Kidude kutengeneza pesa zaidi kwa kufanya maonyesho nchini na nje ya nchi. Katika kipindi hicho, Busara Promotion ilisaidia kukusanya zaidi ya dola 23,000 (36 millions Tsh) kwa ajili ya Bi Kidude katika malipo ya wasanii, ambapo katika kiasi hicho zimebakia dola 2,281 (3, 604,00/- Tsh) katika akaunti yake. Ofisi ya Busara inazo risiti na kumbukumbu zote za Bi Kidude alipochukua fedha kwa miaka saba. 

Busara Promotions inatangaza wazi kuwa haitoachana na kumtupa kwa vyovyote bibi mpendwa kama ilivyo semwa na mkurugenzi Yusuf Mahmoud.
 
"Wakati tunajuta kwamba baadhi ya watu wanaamini vinginevyo, tunatarajia kutamka na kuthibitisha tena kwamba tunatafuta na kuwafanyia wasanii kutoka Afrika Mashariki, wazanzibar na watanzania vile wanavyotaka wenyewe. Busara Promotion itaendelea kumsaidia Bi Kudude Maisha yote" Busara Promotion iko tayari kuzikabidhi fedha za Bi Kidude kwa mtu wa damu kisheria punde iwezekanavyo kwa ushahidi akiwemo mwanasheria na muwakilishi kutoka serekalini na watu wa vyombo vya habari.

0 comments:

 
Top