RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed
Shein leo amewaapisha viongozi na watendaji katika Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar kufuatia uteuzi alioufanya hivi karibuni.
Katika
hafla hiyo iliyofanyika Ikulu mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi
mbali mbali Dk. Shein alimuapisha Mhe. Shawana Bukheti Hassan ambaye
ameapishwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri asiekuwa na Wizara Maalum.
Miongoni
mwa viongozi waliohudhuria ni Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif
Sharif Hamad, Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Balozi Seif Ali Idd, Spika wa
Baraza la Wawakilishi Mhe. Pandu Ameir Kificho, Waziri wa Nchi Afisi ya
Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Mwinyihaji Makame
Wengine
ni Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Mohammed Aboud,
Waziri wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati Mhe. Ramadhan Abdalla Shaaban,
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdillahi Jihad Hassan, Mkuu wa Mkoa wa
Mjini Magharibi Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis, Meya wa Manispaa ya Mji wa
Zanzibar, Mstahiki Khatib Abdulrahman Khatib pamoja na viongozi wengine.
Wakati huo huo,
Dk. Shein amewaapisha viongozi wengine akiwemo Naibu Waziri wa Kilimo
na Maliasili Mhe. Mtumwa Kheir Mbarak pamoja na Naibu Waziri wa Mifugo
na Uvuvi Mhe. Mohamed Said Mohamed.
Viongozi
wengine walioapishwa katika hafla hiyo ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara
ya Miundombinu na Mawasiliano Bwana Tahir M. Abdalla pamoja na Bwana
Mustafa Aboud Jumbe ambaye ambae ameapishwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano.
Pia,
Dk. Shein amemuapisha Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi anaeshughulikia Idara Maalum za SMZ, CDR Julius
Nalimy Maziku pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais (Fedha,
Uchumi na Mipango ya Maendeleo) Bwana Juma Ameir Hafidh.
Hapo
juzi, Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein alifanya mabadiliko ya viongozi na
watendaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kutumia uwezo aliopewa
chini ya vifungu vya Katiba ya Zanzibar ya mwaka
1984 ambapo pia, alifuta rasmi uteuzi wa Mhe. Mansoor Yussuf Himid kuwa
Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi kuanzia Oktoba 15 mwaka huu na Mhe.
Shawana Bukheti Hassan aliteuliwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi.
Rajab Mkasaba, Ikulu
0 comments:
Post a Comment