Biashara ya utalii kkwenye visiwa vya Zanzibar  ni miongoni mwa vitega uchumi ambavyo kwa sasa sekta hii inaonekana kunawiri katika kila pembe ya visiwa vya Zanzibar, ingawaje bado maisha na hali wa watu waishi kando kando ya hoteli bado wapo katika hali ngumu kinyume na matarajio na ndoto zao za kimaisha.
 Kuimarika kwa SEKTA hii ya utalii kwenye visiwani vya Zanzibar inaonekana ni jambo la faraja  kwani, imepelekea vijana wengi wa waishio ndani na nje ya visiwa hivi kuweza kupata ajira, ingawaje bado si ajira rasmi, kwani mara nyingi ajira hii hutegemuea msimu kinyume na hapo vijana wengi huishia vijiweni, huku wakifikiria kitu cha kufanya ili kujikimu kimaisha.
 Hapana shaka yoyote zipo sababu nyingi ambazo zimepelekea  kuimarika kwa sekta hii, ambayo nathubutu kusema kwamba ndio uti wa mgongo na tegemeo la uchumi si tu kwa wananchi bali hata kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ingawaje bado kunahitajika mipango imara ya kuendeleza sekta hii ya utalii visini Zanzibar.
 Katika mataifa mengi ulimwenguni sekta ya utalii huwa ni moja wapo katika ya vyanzo vya kuonegeza au kuinua uchumi wa nchi husika na hasa inatizamiwa kwa mwananchi kwani wao ndio walengwa hasa sekta hii, ingawaje ni vigumu kwa nchini kama Tanzania kesema kwamba sektabhii imekuwa bado ni kitendawili kisicho na mteguaji, hii ni kutokana kwamba bado faida ya utal;ii nchini ni ndogo kulinganisha na mataifa mengine ulimwenguni.
 Nakubaliana na juhudi za  Serikali ya Zanzibar iemkuwa ikifanya juhudi kubwa katika ili kuhakishan sekta hii inakuwa na yenye kuleta tija kwa taifa na wananchi wake kwa ujumla na ndio maana kwa njia juhudi kubwa za SMZ kwa sasa ni kuhakikisha kwamba, ujenzi wa  barabara ziendezo katika maeneo ya utalii kama vile Nungwi, Kiwengwa, Jambiani, Mchanga Mle na maendeo mengine zinaimarika na kuwa bora zaidi ili kila mtu aweze kufika bila ya tatizo lolote, hii ni mikakati bora ya kuimarisha utalii si tu wa nje lakini hata wa ndani pia.
Ifahamike kwamba kuwepo kwa barabara zenye viwango vionavyotambulika  kwa mujibu wa Mkandarasi iwezesha watalii watembeleao  Zanzibar kutokuwa na mashaka wala wasi wasi wowote katika safari zao za kuelekea Kiwengwa ama Nungwi kwani huwa wanafika kwa wakati unaotakiwa.
 Lakini pia kuwepo kwa barabara zilizojengwa vyema  imepelekea hata wenyeji wa maoneo ya utalii kuweza kufanya shughuli zao bila ya khofu na hasa wakati  wanapopoleka mazo yao  katika hoteli na maeno mengine ya mji wa Zanzibar kwa ajili ya kutafuta soko zaidi la bidhaa zao ambzo kuuza kwao ndio manufaa kwao na jamaa zao, lakini pia hata kuimarika kwa kipatop cha mtu mmoja mmoja na serikali kwa ujumla.
Ifahamike kwamba hapo awali bara bara nyingi za vijiji vya Unguna na Pemba zilikuwa katika hali mbaya kitu ambacho kilipelekea kudumaza hata maaendelea ya watu waishio vijini.
 Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar Ali Khalili Mirza ameeleza kwamba kwa sasa, sekta ya utalii kwa uapande wa Zanzibar imekuwa kwa kasi sana,  kutokana na mikakati thabiti iliyowekwa na Serikali ya Zanzibar, kwa kushirikina na wahisani  mbali mbali wa maendeleo kwa ajili ya kuinua uchumi wa nchi na maendeleo kwa ujumla.
 Katibu Mirza  alieleza kwamba  kuimarika kwa barabara za Zanzibar pamoja na  ujenzi wa hoteli za kisasa katika fukwe za bahari ya Zanzibar, imekuwa ni kuvutio kikubwa cha wageni kuitembelea Zanzibar mara kwa mara lakini pia hata wananchi wenyewe wamekuwa wakitembelea sehemu mbali mbali za fukwe za Zanzibar kila ifikapo mwishoni mwa mwezi.
 Mirza alisema kwamba katika mwaka 1987 Zanzibar  kulikuwa na hoteli zisizo zidi  94 na sasa zipo zaidi ya hizo kutokana na jitihada kubwa ya Serikali ya Zanzibar na watu wake,  ambapo kwa kiasi kikubwa Serikali ya Zanzibar iliweza kujenga mazingira  mazuri ya uwekezaji ambayo yamepelekea kuongezeka kwa ujenzi wa  mahoteli na kufikia 141.
 Hata hivyo, Mirza alifahamisha kwamba, tangu kuimarika kwa ujenzi wa barabara zilizopo kwenye vijiji vingi za Zanzibar na hasa kwenye maeneo ya kitalii, ujenzi wa mahoteli nao umekuwa na mahoteli na kupelekea kuongezeka kwa  idadi ya wageni(watalii)  wanaotembelea  Zanzibar na kufikia watalii 175,067 mwaka 2011  kutoka watalii 19,368 mwaka 1985.
 Kwa uapande wake, Meneja wa hoteli ya Zanzibar Beach Resort  Farid Abdalah akieleze kuhusu  kukua kwa sekta hiyo alisema, mafanikio hayo yametokana na kuwepo kwa hali ya amani na utulivu kwenye visiwa vya  Zanzibar ikiwa ni  pamoja na kuimarika kwa barabara zake, bandari pamoja na uwanja wa ndege.
 " Kwa sasa tunashukuru Mungu kwa kuwa kuna mazingira ya amani visiwani humu ambapo imepelekea sekta ya utalii kupanuka  kutokana na kuongezeka kwa mashirika mbali mbali ya ndege sasa yanayofanya safari zake Zanzibar" alisema Farid.
  Wakitoa maoni yao baadhi ya vijana wanaofanya kazi ya kuwaongoza watalii (tour guide) walisema kwamba kwa sasa wameweza kunufaika vyema na  na kazi ya utalii ambayo kwa sasa ndio muhimi mkuuu wa na dira ya maisha yao ya kila siku kuliko kuendela kukaa vijiweni ambako hakuna manufaa yoyote kwao na kwa jamii kwa ujumla.
 Aidha wimbi kubwa la vijana ambao hutoka nje ya nchi hufika Zanzibar kwa ajili ya kutafuta ajira na hufakiwa kuchukuwa ajira kiulani katika sekta ya utalii, hii ni kwa sababu hapo awali vijana wengi wa Kizanzibar walikuwa hawapo tayari kuingia kwenye sekta hii ya utalii lakini kutokana na ukata wa maisha unaoikabili taifa vijana wengi waishio visiwani humu nao sasa wamekuwa mstari wa mbele katika sekta hii ya utalii.

0 comments:

 
Top