Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif Ali Iddi ameupongeza Umoja wa Mataifa { United Nation } kwa kutimia
miaka 67 tokea kuasisiwa kwake mnamo mwaka 1945.
Balozi Seif alitoa pongezi hizo
wakati akisalimiana na Ujumbe wa Shirika
la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo { UNDP } hapo Ofisini kwake katika
Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Ujumbe huo wa Shirika la Mpango wa
Maendeleo la Umoja wa Mataifa ulioongozwa na Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa
Mataifa aliyepo Nchini Tanzania Bwana Alberic Kacou
uliambatana pia na Mwakilishi wa Shirika hilo aliyepo Zanzibar Bibi Anna Senga.
Balozi Seif alisema Umoja huo umeundwa
maalum kwa lengo la kutoa huduma itakayokidhi mahitaji ya Mataifa yote Wanachama wa Umoja huo hasa
katika masuala ya kustawisha Amani na ustawi wa Jamii.
Alieleza kwamba Taasisi zilizoundwa
chini ya mwamvuli wa Umoja huo zimekuwa zikiendelea kutoa huduma mbali mbali
kwa Mataifa Wanachama zilizopelekea kupiga hatua kubwa za Maendeleo hasa katika
Nchi za Dunia ya Tatu.
Alisema Jamii za Kimataifa zimekuwa
zikishuhudia ufanisi huo hasa katika miradi ya Afya, Chakula na lishe, Maji,
sambamba na kudhamini Mafunzo ya Elimu ya Uraia kwa lengo la kutandika
Demokrasia Duniani.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
aliueleza Ujumbe huo wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa kwamba Zanzibar bado inahitaji kuendelea kuungwa
mkono na Taasisi za Umoja huo katika harakati zake za Maendeleo na Ustawi wa
Jamii.
Alifahamisha kwamba mradi wa huduma
za maji safi na salama katika maeneo mbali mbali ya Visiwa vya Unguja na Pemba
umepewa kipaumbele katika jitihada za kuweka miundo mbinu.
Aliutaka Uongozi wa Taasisi hizo za
Umoja wa Mataifa licha ya juhudi zinazoendelea kuchukuwa za kuiunga mkono
Zanzibar lakini bado ina nafasi ya kusaidia miradi mengine katika Sekta ya
Elimu, Kilimo sambamba na Elimu ya Uraia { Sivic Education }.
Mapema Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa aliyepo Nchini Tanzania Bwana Alberic Kacou alimueleza
Balozi Seif kwamba Umoja huo kupitia Mashirika yake ya Umoja huo
{ UNDP } yatajitahidi kuendelea
kuangalia mazingira ya kusaidia sekta ya Afya, Chakula na Lishe.
Bibi
Anna Senga anatarajiwa kufanyia kazi zake za Shirika la Mpango wa
Maendeleo ya Umoja wa Mataifa { UNDP }
Hapa Zanzibar ambae ni mwakilishi wa Shirika hilo.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar
0 comments:
Post a Comment