Msimamizi
wa Kituo cha Afya cha Kendwa Nungwi Bwana Viola Franco kutoka Hoteli ya
Kimataifa ya Lagema Nungwi inayosimamia Kituo hicho akimkaribisha Balozi Seif
Ali Iddi wakati alipofanya ziara ya kukitembelea Kituo hicho kipya kuona huduma
zinazotolewa
Uongozi wa Wizara ya Afya Zanzibar umeagizwa kuandaa
Mpango Maalum kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali kubwa ndani ya Wilaya ya Kati
itakayosaidia kuipunguzia msongamano mkubwa wa Wagonjwa Hospitali
Kuu ya Mnazi Mmoja.
Agizo hilo limetolewa
na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi
Seif Ali Iddi alipokuwa akiendelea na awamu ya pili ya ziara yake ndani ya
Taasisi za Wizara ya Afya hapa Zanzibar.
Balozi Seif aliueleza Uongozi wa Wizara hiyo ya Afya
kwamba Serikali Kuu itakuwa tayari kuangalia uwezekano wa uwezeshaji wa ujenzi
wa Hospitali hiyo muhimu kwa Jamii.
“ Tumefikia wakati kulingana na mahitaji ya huduma za
Afya kwa wananchi wetu kuwa na Hospitali kubwa katika kila Wilaya na hii kwa kiasi kikubwa itaondosha vurumai
isiyo ya lazima katika Hospitali yetu ya Rufaa ya Mnazi Mmoja”. Alisisitiza
Balozi Seif.
Balozi Seif alisema katika kukabiliana na changamoto zinazoikabili Hospitali Kuu ya
Mnazi Mmoja ameahidi kusaidia Vitanda 10 kwa ajili ya wodi ya Wazazi na
Serikali itajitahidi kutafuta mbinu za kutatuta changamoto chengine zilizopo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliwapongeza
Watedaji wa Hospitali hiyo kwa utendaji wao wa kazi licha ya mazingira magumu wanayofanyia
kazi.
Balozi Seif alishuhudia idadi kubwa ya Wagonjwa
wanaopata huduma katika Hospitali hiyo ambapo Mkurugenzi wa Hospitali Kuu ya
Mnazi Mmoja Dr. Jamala Adam alieleza
kwamba uwezo wa kuhudumia wagonjwa bado ni ule ule tokea miaka ya thamanini
wakati idadi ya wagonjwa imeongezeka mara dufu.
Akiitembelea Hospitali ya Wazazi ya Muembe Ladu Balozi
Seif alielezwa na Watendaji wa Hospitali hiyo mfumo mpya ulioanzishwa wa makuzi
ya mtoto kwa yule aliyezaliwa akiwa pungufu wa uzito ujuilikanayo kwa jina la
Kangaroo.
Mafunzo hayo tayari yameshaanza kufundishwa kwa Wazazi
mbali mbali kwa lengo la kujiweka tayari endapo Mzazi atatokezewa kujifungua
Mtoto mpungufu.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alikagua utendaji wa
wafanyakazi wa Hospitali ya Kivunge ambapo Muuguzi mkuu wa Hospitali hiyo Dr.
Ashura Shaib Mussa alishauri kuwepo kwa Kitengo cha Upasuaji ili kuwapunguzia
hatari wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo ya ghafla.
Dr. Ashura alisema ipo hatari na inaweza kusababisha kifo kwa mzazi anayehitaji
operesheni ya ghafla kwa kumsafirisha katika masafa marefu kupatiwa huduma
hiyo.
Akizungumza na Watendaji hao Balozi Seif aliwapongeza
Madaktari, Wauguzi pamoja na Wafanyakazi wote wa Hospitali ya Kivunge kwa
juhudi zao za kuiwekea mazingira safi
Hospitali hiyo.
Balozi Seif aliahidi kuipatia Hospitali hiyo Vitanda
kumi na kuwataka wajenge utamaduni wa kuvifanyia majaribio Vifaa vipya
wanavyopelekewa hata kama itakuwa bado
kuvifanyia kazi pamoja na kuyapatia changa moto matatizo yanayowakabili.
“Kama sijajua
matatizo na changamoto zilizomo ndani ya Mawiza na Taasisi za Serikali wakati
mimi ndie Mtendaji Mkuu wa Serikali nitashindwa kutoa maamuzi au ufafanuzi pale
unapohitajika”. Alisema Balozi Seif.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimalizia ziara yake kwa kukaguwa
Hospitali mpya ya Wazazi iliyopo katika Kijiji cha Kendwa ambayo imefadhiliwa
na Uongozi wa Hoteli ya Kimataifa ya Lagema. Daktali Mkuu wa Hospitali hiyo
iitwayo R.G.F Matenity Clinic Dr. Hawa Kivembele alimueleza Balozi Seif kwamba
huduma za Hospitali hiyo ambazo ni bure zilizoanza mapema mwezi huu zimelengwa
kwa wanakijiji wa eneo hilo.
Hata hivyo Dr. Hawa alisema mbali ya wanakijiji hao
lakini pia Hospitali hiyo hutoa huduma ya malipo kwa Wafanyakazi wa Hoteli zote
zilizoko katika Othman Khami Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
0 comments:
Post a Comment