Maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012 Nchini yanaendelea vyema kulingana na ratiba ya utekelezaji licha ya changamoto ndogo ndogo zilizopo hivi sasa. Hilo lilifahamka katika Kikao cha Tano cha Kamati Kuu ya Tifa ya Sensa ya Watu na Makazi kilichofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kibaha chini ya MwenyekitiMwenza wa Kmati hiyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi. Miongoni mwa changamoto zilizotajwa katika kikao hicho ni kwa baadhi ya Viongozi wa Dini ya Kiislamu kuendelea kuhamasisha waumini wao kutoshiriki katika zoezi la sense kwa madai ya kutoingizwa kwa swali la Dini kwenye madodoso ya Sensa. Akitoa Taarifa ya maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi kwa upande wa Tanzania Bara Naibu Waziri wa Fedha wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Saada Mkuya alisema hatua za maandalizi hayo zinaendelea na sasa zimeingia katika hatua muhimu ya kuelekea kipindi cha kuhesabu Watu. Mh. Saada alisema wakala wa Majengo tayari ameshakamilisha matengenezo ya jengo la kuingizia Takwimu kwenye kompyuta sambamba na uwekaji wa umeme kazi inayotarajiwa kukamilika gosti 15 mwaka huu. Alisisitiza kwamba utekelezaji wa tathmini ya sense utaanza mara baada ya kukamikika kwa zoezi la kuhesabu watu mwezi septemba mwaka 2012 ikitanguliwa na Kamati ya Kitaalamu ya Sensa kupitia madodoso, miongozo na sampuli itakayotumika wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo. Naibu Waziri wa Fedha wa Muungano Mh. Saada alifahamisha kwamba Serikali imeshatoa kiasi cha shilingi Bilioni 22.5 kwa ajili ya uhamasishaji, mafunzo ya wakufunzi ngazi ya Mikoa pamoja na ununuzi na usafirishaji wa vifaa kupelekwa Mikoani. Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo Zanzibar Mh. Omar Yussuf Mzee alisema kwa upande wa Zanzibar matayarisho ya Sensa yako katika hatua ya za mafunzo kuelekea kipindi muhimu cha kuhesabu watu. Mh. Omar alisema shughuli za uhamasishaji pia zimefikia hatua nzuri kwa kupitia na kushirikishwa Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar kwa kuendelesha Mikutano na Viongozi wa Dini. Alisema shughuli hiyo pia imekwenda sambamba na maandalizi ya matangazo, vipindi vya uhamasishaji katika Taasisi za Habari pamoja na michezo ya kuigizwa inayoandaliwa na wasanii maafuru nchini. Mapema Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu { UNFPA } Bibi Mariam Khan ambae alipata fursa ya kutoa salamu katika kikao hicho alisema Dunia wakti wote inahitaji kuwa na Takwimu sahihi ya idadi ya watu kwa Maendeleo ya Ustawi wao Kiuchumi na Ustawi wa Jamii. Bibi Mariam alisema Shirika hilo litaendelea kushirikiana na Tanzania ikiwa ni miongoni mwa Nchi 140 Duniani zinazopata huduma kutoka shirika hilo katika harakati za makusanyo ya Takwimu ili kuwa na uhakika wa mipango sahihi ya Maendeleo. Mwenyekiti Mwenza wa Kikao hicho cha Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi Balozi Seif Ali Iddi alilipongeza Shirika hilo la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu { UNFPA } kwa hatua zake za kuunga mkono Maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi ya Tanzania mwaka huu wa 2012. Balozi Seif alisema hatua ya Shirika hilo hasa katika masuala ya uwezeshaji na Taaluma imewawezesha watendaji wa Kamati ya Sensa na zile za Takwimu bara na Zanzibar kuendelea kufanya kazi kitaalamu zaidi. Mapema Mwenyekiti huyo mwenza wa Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa Balozi Seif Ali Iddi alielezea kuridhika kwake na hali nzuri ya Kituo kikuu cha Vifaa vya Sensa kilichopoKibaha ambacho kinaendelea na matengenezo ya mwisho. Alisema kazi kubwa iliyopo hivi sasa ni kwa viongozi kuendelea kuhamasisha Wananchi umuhimu wa kujiandaa kwa ajili ya uandikishaji wa sense wakati za zoezi utakapowadia.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

0 comments:

 
Top