Jamuhuri ya Watu wa China imeahidi
kuendelea kuiunga mkono Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika harakati zake
za Maendeleo , Uchumi na hata Maafa na Majanga wakati yanapotokea. Wito huo umetolewa na Balozi Mdogo wa
China aliyepo Zanzibar Bibi Sheen Limun wakati wa mazungumzo yake na Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyekwenda kumpa pole kufutia
maafa ya ajali ya Meli ya M.V Skagit iliyotokea Jumanne iliyopita karibu na
Kisiwa cha
Chumbe.
Balozi Sheene aliambatana na Uongozi wa
Kampuni za Ujenzi za China zinazofanya kazi hapa Zanzibar za Railway Jiangchang
Engineering Co Ltd na ile ya Beijing Construction Engineering Group ambazo zote
zimekabidhi mchango wa shilingi milioni tano kila moja kusaidia Mchango wa
Maafa hafla iliyofanyika katika Ofisi ya Spika wa Baraza la Wawakilishi Mbweni
nje kidogo ya Mji wa Zanzibar .
Alisema Wananchi wa Jamuhuri ya Watu wa China wanajua hali ya huzuni
iliyoikumba Jamii ya Watanzania hasa wazanzibari kutokana na msiba huo wa
kuzama kwa Meli iliyosababiha vifo vya wananchi waliyomo kwenye boti hiyo.
Balozi Sheen alimhakikishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kwamba ushirikiano wa wa kihistoria kati ya pande hizo mbili utaendelea kudumishwa kwa hatma ya Nchi hizo mbili.
Balozi Sheen alimhakikishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kwamba ushirikiano wa wa kihistoria kati ya pande hizo mbili utaendelea kudumishwa kwa hatma ya Nchi hizo mbili.
Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili
wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliipongeza Serikali ya Jamuhuri ya
Watu wa China kupitia Balozi zake Nchini Tanzania kwa jitihada zake za kuunga
mkono Harakati za Maendeleo hapa
Nchini.
Balozi
Seif alimueleza Balozi Mdogo wa China Aliyepo Hapa Zanzbar kwamba Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar imeanza kuchukuwa hatua mbali mbali za kujihami au
kuwepuka Maafa wakati yanapotokezea
Majanga.
Alisema Serikali kupitia ushirikiano wa pamoja
wa Mamlaka za Usafiri wa Baharini za Bara { Sumatra} na ile ya Zanzibar { ZMA }
zitawajibika kuvifanyia uchunguzi vyombo vyote vya usafiri wa Baharini kila
muda kwa vile vitavyoruhusiwa kutoa huduma hiyo
“ Wamiliki wa Vyomo vya Usafiri wa
Baharini lazima wafuate sheria na Taratibu za Mamlaka ya usafiri wa Baharini
kwa lengo la kuwepuka maafa yanayoweza kukingika”. Alisisitiza Balozi Seif
Aidha Balozi Seif aliongeza kwamba
taratibu zitaendelea kuimarishwa ili kuona Mwekezaji anayeagiza vyombo
vya Usafiri wa Baharini anawasilisha vielelezo vyake vya chombo husika kwanza
kabla ya kuagiza ili kufanyia uhakiki wa kitaalamu
Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alikutana naMkurugenzi anayeshughulikia
Masuala ya Afrika na Carribean wa Umoja wa Ulaya { EU } Bibi Fransisca Mosca
hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar
Katika mazungumzo yao Balozi Seif
aliuomba Umoja huo wa Ulaya kuangalia uwezekano wa kusaidia juhudi za Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar za kutafuta mbinu za upatikanji wa usafiri wa uhakika
kati ya Unguja na Pemba.
Alisema Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar inakudia kuwa na Meli zake kama kawaida baada ya zile zilizokuwa zikutumika
kupitwa na muda wake wa matumizi
Naye Mkurugenzi huyo anayeshughulikia
masuala ya Afrika na Carribean Bibi Fransisca Mosca alimuhakikishia Balozi Seif
kwamba ushirikiano wa muda mrfu uliopo kati ya Umoja huo na Zanzibar na
Tanzania kwa ujumla utaendelezwa.
Othman Khamis
Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
0 comments:
Post a Comment