Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara Afrika {CBA} Bw. Yohane Kaduma akikabidhi mchango wa Maafa kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar balozi Seif Ali Iddi kufuatia ajali ya Meli ya M.V. Skagit hivi karibuni.
Benki ya Biashara ya Afrika { CBA } inajaribu kuangalia utaratibu wa namna itakavyoweza kusaidia kutoa mkopo ili kuchangia kufanikisha azma ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya ununuzi wa Meli kubwa ya kusafirishia Abiria na Mizigo.
Kauli hiyo imetolewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Bwana Yohane Kanuma wakati akiwasilisha mchango wa Maafa kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Bwana Yohane alimueleza Balozi Seif kwamba Taasisi yao haina sababu ya kutochangia suala hilo ili kujaribu kusaidia nguvu za kuepuka majanga yanayoweza kukingika ndani ya Sekta ya Usafiri wa Baharini.
Alisema kitakachozingatiwa zaidi ni jinsi gani pande hizo mbili yaani Benki hiyo na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zitakavyofikia makubaliano ya masharti ya mkopo utakaokubalika kutolewa na Benki hiyo.
Afisa Mtendaji Mkuu huyo wa CBA alifahamisha kwamba Jamii kupitia Viongozi wa Taasisi inapaswa kuendelea kuwa makini katika kulinda roho za Raia kwa hali yoyote ile ambayo imo ndani ya uwezo wao.“ Tunapaswa kuwa makini katika kulinda Maisha ya Watu kwani hakuna fedha wala mali inayoweza kulipa roho za Watu”. Alisisitiza Bwana Yohane.
Alizitaka Familia zilizopatwa na misiba ya Jamaa zao katika ajali hiyo ya Meli ya M.V. Skagit kuwa na moyo wa subra katika kipindi hichi kigumu cha maombolezo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiangalia Hundi ya mchango wa maafa iliyotolewa na  Meneja wa Shirika la Bima ya Afya Tanzania Bwana Peter Daniel hapo Ofisini kwake Baraza la Wawakilishi Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar
Kwa upande wake Meneja wa Shirika la Bima ya Afya Tanzania Bwana Peter Daniel akikabidhi mchango wa Maafa kwa Balozi Seif alisema Uongozi wa Shirika hilo umeguswa na Janga hilo lililopelekean kupotea kwa roho za Watu kadhaa hapa Nchini.
Bwana Peter alifahamisha kwamba mchango wao licha kwamba ni mdogo lakini unaweza kuwa chachu ya kuungana na familia zilizopatwa na isiba hiyo katika kupunguza machungua hayo
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akipokea mchango wa maafa kutoka kwa Mwakilishi wa Kampuni ya Jman Investiment inayotoa huduma katika Viwanja vya Ndege Bwana Qovirvi Sandrudi
Kwa upande wake Mwakilishi wa Kampuni ya Jaman Investiment inayotoa huduma katika Viwanja vya ndege Bwana Qovirvi Sadrudin akitoa mchango wa Maafa alizitaka Familia za Watu waliofiwa na wale waliopotelewa na jamaa zao kuwa wavumilivu.
Bwana Sandrudin alisema huo ni msiba mzito ambao unamgusa kila mwana jamii ndani ya Taifa hili la Tanzania.
Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliendelea kusisitiza kwamba Serikali imeshafanya maamuzi ya kununu Meli Mpya za Usafiri wa Abirina Mizigo kwa uhakika na salama.
Alisema hatua za makusudi zitaendelea kuchukuliwa katika suala zima la kukabiliana na Maaafa wakati yanapotokezea yale ya bahati mbaya na si uzembe.
“ Katika kukabiliana na Maafa tutajitahidi zaidi hata kama wenzetu wengine watatuona wabaya”. Alifafanua Balozi Seif.
Balozi Seif alifahamisha kwamba Serikali imeaanza kuonyesha njia ambayo wengine lazima waifuate kwa kuizuia Meli yake ya Serikali ya M.V. Maendeleo kutofanya kazi mpaka ikaguliwe na Taasisi za Mamlaka ya Usafiri licha ya kurejea hivi karibuni matengenezoni Nchini Kenya.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliendelea kuzipongeza Taasisi zote zinazojitolea kutoa misaada yao ambayo itasaidia hatua zote za kukabiliana na janga hilo kubwa.
Othman Khamia Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

0 comments:

 
Top