Uongozi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Tanzania
{costech} umeombwa kushajiisha Wasomi hasa Vijana wa Vyuo Vikuu Nchini kupenda
kufanya tafiti mbali mbali zitakazojenga Mazingira ya kumuondoa Mtanzania kwenye matatizo yanayomkabili.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif Ali Iddi ametoa ombi hilo
katika Hafla fupi ya uzinduzi wa Ofisi ya Tume hiyo ilyofanyika hapo Tunguu
Mkoa wa Kusini Unguja.
Balozi Seif alisema Tafiti kama
hizo ambazo zitakuwa na uhusiano wa moja kwa moja na Mwananchi zinaweza kusaidia kupata Maendeleo kwa kasi
zaidi katika Kipindi kifupi kijacho.
Alisisitiza kwamba Serikali kwa upande wake iko tayari
kwa namna yoyote ile kutumia vyema matokeo ya Tafiti zinazofanywa na Wazomi
wazalendo.
Hata hivyo Balozi Seif alieleza kuwa yapo baadhi ya
matokeo ya Tafiti hubakia kuwa siri kwa Taifa lakini mengine yanastahiki
kutolewa kwa Wananchi ili waelewe kinachoendelea kwenye maisha yao.
Balozi Seif alieleza kwamba wakati umefika kwa
Makampuni pamoja na Viwanda vya hapa Nchini kujenga Utamaduni wa kutoa kazi zao
za Utafiti kwa Tume hiyo ili ijipatie fedha za kuendesha shughuli zake za
utafiti kama Nchi nyengine zilizoendelea.
Alieleza kwamba Tanzania imepania kuleta maendeleo
kwa Wananchi wake kutokana na uamuzi wake wa kutenga Jumla ya shilingi za
Kitanzania Bilioni Thalathini { 30,000,000,000/-} kwa ajili ya Utafiti na
Maendeleo kwenye Bajeti yake ya Mwaka 2010/2012.
Balozi Seif alifahamisha kwamba Maendeleo bila ya
Sayansi na Teknolojia hayapatikani kwani
masuala hayo mawili yanakaribiana katika utekelezaji wake.
Akizungumzia Tume ya Taifa ya nguvu za Atomu Balozi
Seif alielezea kufarajika kwake kutokana
na mipango m,izuri ya Taasisi hiyo kuhudumia Zanzibar katika masuala ya usimamizi wa matumizi
salama ya Mionzi.
Balozi Seif alisema ushirikiano wa pamoja wa Taasisi
hiyo,Wizara ya Afya Zanzibar na Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani katika
kuanzisha mradi wa Matibabu ya Saratani
katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja unafaa kuungwa mkono.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi ameishukuru Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uamuzi wake
wa wa kusogeza karibu na Wananchi
shughuli za Ofisi ya Tume ya Taifa ya
Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Tume ya Taifa ya Nguvu za Atomu.
Katika Taarifa yake Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu
za Atomiki Tanzania
Profesa Iddi Suleiman Nyangarika Mkilaha alisema Taasisi yake itaendelea kutoa
Elimu sahihi ya matumizi ya Mionzi.
Profesa Nyangarika alisema Taaluma hizo kwa sasa
itazingatia zaidi katika sekta ya Viwanda pamoja na Vituo vya Afya ambavyo
vinatumia Vifaa vyenye mazingira ya Nguvu za Atomiki.
Mkurugenzi huyo wa Tume ya Nguvu za Atomiki alifahamisha
kwamba katika kupanua zaidi huduma zake Taasisi hiyo itaendelea kupima Mionzi
katika Mimea ili kujua kiwango sahihi cha kulinda Vyakula kwa ajili yamatumizi
bora kwa Wanaadamu.
Mapema Waziri wa Mawasiliano,Sayansina Teknolojia wa
Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Makame Mnyaa Mbarawa alisema
Wizara hiyo itaendelea kushirikiana na Wataalamu wa ndani na nje ili kuona
Tafiti zinazofanywa zinatmika kwa walengwa ambao ni Wananchi.
Alisema Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia na ile
ya Nguvu za Atomiki zimeanzishwa zikiwa na wajibu wa kusimamia tafiti na nguvu
za Atomiki Nchini kwa kushirikiana na Taasisi za Kanda na zile za Kimataifa.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Mkamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
0 comments:
Post a Comment