Vijana ndani ya Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake
wamesisitizwa kuendelea kutunza amani iliyopo na kujiepuka na shari inayoweza
kuzaa balaa na hatimae kuzagaa kwa maafa Nchini.
Sisitizo hilo limetolewa na Mjumbe wa Kamati ya Siasa
ya CCM ya Wilaya ya Kaskazini B ambaye pia ni Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi wakati
akiufungua Mkutano Mkuu wa Umoja wa Wapanda Mapiki Pili wa Wilaya hiyo hapo Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya CCM Jimbo la
Kitope uliopo Kinduni.
Mama Asha amesema Vijana hao wanapaswa kuwa waangalifu
zaidi kutokana na vitendo vinavyoashiria fujo
ambavyo huonekana kukumba zaidi kundi kubwa la Vijana.
Amesema suala la utunzaji wa Amani linamuhusu kila
Mwana Jamii kwani hata Dini zote pamoja na Madhehebu mbali mbali zimekuwa zikihubiri
na kuhimiza suala la utunzwaji wa Amani.
Akizungumzia suala la Uchaguzi Mama Asha aliwahimiza
Wajumbe wa Mkutano huo kuhakikisha Wanawachaguwa Viongozi Makini watakaokuwa
Mahiri kwenye uendelezaji wa Ushindi wa Chama chao Katika Uchaguzi ujao.
Alisema Tabia ya Baadhi ya Watu kuchagua Viongozi kwa
misingi ya Ukabila na kujuana imepelekea kukitia doa kubwa Chama Hicho ambacho
ndio kimbilio la Wanyonge Nchini.
“ Ukweli tabia hii mbaya sana inakera na inafaa kuepukwa mara moja kwa
vile inapunguza kwa kiasi kikubwa nguvu ya Chama ”. Alisisitiza Mama Asha.
Mama Asha aliwakumbusha Vijana hao kuendelea kuyatetea
Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 1964 ambayo
yalileta faraja kwa Wananchi walio wengi hapa Zanzibar.
Alisema Vijana wanapaswa kuwa makini katika kutetea
Viongozi wao kutokana na tabia ya baadhi ya watu kuendeleza tabia ya kuhubiri Matusi
hadharani hana sababu dhidi ya Viongozi hao.
Katika kuunga Mkono juhudi za kuendeleza Umoja huo wa
Wapanda Mapiki Piki wa Wilaya ya Kaskazini B Mama Asha amechangia jumla ya
Shilingi Laki Tatu Taslimu { 300,000/- } kusaidia kutunisha Mfuko wa Umoja huo.
Katika Risala yao
iliyosomwa na Katibu Msaidizi wa Umoja huo Nd. Ame Pandu Kombo Vijana hao
wameahidi kuendelea kuhamasisha Wananchi pamoja na Wanachama katika kuunga
mkono Sera za Chama Tawala ambacho ndio kimbilio la Wananchi walio wengi
Nchini.
Nd. Ame alisema Umoja wao licha ya kazi kubwa
wanayoendelea kuitekeleza lakini bado wanakabiliwa na Changa moto mbali mbali zinazokwamisha
kutekeleza majukumu yao.
Alizitaja Changa moto hizo kuwa ni pamoja na ufinyu
wa sare wakati wanapokuwa katika shughuli zao za uhamasishajipamoja na Mtaji mdogo wa Umoja wao unaopelekea kushindwa
pia kufungua Akaunti Benki.
Mapema akimkaribisha Mgeni Rasmi kufungua Mkutano huo,
Mwenyekiti wa Umoja wa Wapanda Mapiki Piki Wilaya ya Kaskazini B Nd. Mosi Ame
Mosi aliwatahadharisha Vijana hao kuwa mbali na Makundi ya sasa
yanayopandikizwa cheche za kuchafua amani ya Nchi katika maeneo mbali mbali
hapa Nchini.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
0 comments:
Post a Comment