Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema mchango mkubwa wa Msanii Steven Kanumba ambao alikuwa akiutoa wakati wa uhai wake ndani ya Tasnia ya Filam umeanza kuwa tegemeo la uchumi ndani ya Taifa la Tanzania.
Balozi Seif alieleza hayo katika barua yake ya rambi rambi aliyompelekea Waziri wa Habari, Vijana na Michezo Tanzania Bara Dr. Emmanuel John Nchimbi kufuatia kifo cha Msanii kanumba kilichotokea usiku wa Kuamkia Tarehe 7 March mwaka huu.
Alisema Matukio tofauti ya Maisha aliyoyaigiza Msanii kanumba kwenye michezo yake yaligusa hisia za Watu wengi ndani na nje ya Nchi jambo ambapo pia limewezesha fani hiyo kutoa ajira kubwa na kuongeza mapato ya Taifa.
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar alisema taarifa ya kifo cha ghafla cha Marehemu Kanumba kimesikika na kupokewa kwa masikitiko na wapenzi wengi wa fani ya sanaa Nchini.
Balozi Seif alisisitiza kwamba Marehemu Kanumba kwa kweli alikuwa msanii wa watu na atabakia hivyo ndani ya nyoyo za wapenzi wake milele.
Aliongeza kwamba kifo hicho kimeacha pengo kubwa sio tu kwa familia bali pia kwa Taifa hasa katika kasnia ya Filam ambayo katika mchango wake imekuwa tegemeo la uchumi.
Balozi Seif alisema kwa niaba yake na Serikali ya Mapinduzi uya Zanzibar pamoja na watu wake anawapa pole kwa familia ya marehemu kupitia Waziri Nchimbi.
Aliwataka kuwa na ustahamilivu na subra katika kipindi hichi kigumu cha huzuni na maombolezo.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

0 comments:

 
Top