Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi amesema ni vyema kwa Wanafunzi kuzingatia kuwa misaada inayotolewa na Washirika wa Maendeleo inakuwa chachu kwao katika kujitafuatia elimu itakayowafaa hapo baadaye.
Balozi Seif ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema hayo katika hafla fupi ya kukabidhi vikalio 70 kwa ajili ya ukumbi wa Skuli ya Kitope pamoja na sare 222 kwa wanafunzi wa skuli nne za Jimbo hilo wanaoishi katika mazingira magumu.
Hafla ilifanyika katika Viwanja vya Skuli ya Kitope ambapo Vikalio hivyovimetolewa na Washirika wa Maendeleo vikiwa na Thamani ya Shilingi Milioni 5,000,000/- wakati sare zilifdhiliwa na Taasisi ya Uniform Tanzania zikiwa na Thamani ya shilingi Milioni 3,108,000/-.
Balozi Seif alisema hatua ya Wanafunzi hao kusoma kwa bidii itawapa moyo Wahisani pamoja na Washirika wa Maendeleo kuendelea kusaidia Sekta ya Elimu hapa Nchini.
Mbunge huyo wa Jimbo la Kitope amewapongeza Wafadhili hao kwa juhudi zao za kuchangia Sekta ya Elimu ambayo ni muhimu kwa Kizazi kijacho kutokana na mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia.
Akitoa shukrani kwa Niaba ya Walimu na Wanafunzi wa Skuli zote zilizopata msaada huo Msaidizi Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Kitope Nd. Suleiman Juma Makame alisema bado wanaendelea kuthamini juhudi na misaada inayotolewa na washirika pamoja na Viongozi wao.
Ndugu Suleiman alisisitiza kwamba Jamii inayowazunguuka inafarajika kuona lengo la Viongozi la kutaka kuimarisha sekta ya Elimu linatekelezeka.
Naye Mmoja wa Wafadhili wa Sare za Wanafunzi hao wa Taasisi ya Uniform Tanzania kutoka Nchini Sweden Bibi Agnes Sjoerg alisema lengo la Taasisi yao ni kushajiisha elimu kwa vile ndio Mkombozi wa Mwanaadamu.
Bibi Agnes alisema Wanachama wa Taasisi hiyo ambao ni Wanafunzi Nchin Sweden wamefikia uamuzi wa kuchangishana kwa ia ya kusaidia Wanafunzi wenzao Nchini mbali mbali ambazo zimekuwa na watoto wenye mazingira magumu.
Mapema MBunge wa Jimbo la Kiope Balozi Seif Ali Iddi alikitembelea Kikundi cha Ushoni cha Jimbo la Kitope Kinachoendelea kupata mafunzo ya ushuno hapo katika Ofisi ya CCM jimbo la Kitope.
Balozi Seif katika ziara hiyo aliambatana pamoja na Wawakilishi wa Uniform Tanzania Bibib Agnes Sjobeg, Bibi Sophie Mellstig pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa chuo cha Ushoni Kiliopo Magomeni { Magomeni Modern Tailoring Academy } Ndugu Rashid Makame Shamsi.
Akitoa Salamu zake kwa wanakikundi hao wa Kitope Mkurugenzi huyo wa Modern Tailonring Academy Nd. Rashid alisema uongozi wake utajaribu kuratibu namna ya kutoa Mafunzo kwa Wanakikundi hao ili kuwasaidia zaidi Taaluma ya Ushoni.
Hata hivyo Nd. Rashid alitahadharisha kwamba mafunzo ya ya ushoni yamebadilika na kuwa ya Kitaalamu zaidi jambo ambalo wana kikundi hao wakubali kubadilika.
Alielezea matumini yake kwamba mafunzo hayo mbali ya kutoa uelewa mkubwa zaidi lakini pia yatasaidia kuipunguzia mzigo wa ajira Serikali Kuu kwa vile wao watakuwa tayari wameshajihakikishia ajira ya kudumu.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

0 comments:

 
Top