Azma ya Serikali ya Kuunda Wizara inayosimamia uwezeshaji ni kumfanya Mwananchi ajitegemee kufanyakazi kwa kutumia nguvu kazi badala ya kuwa tegemezi kwa wengine.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alisema hayo wakati akizunguma katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya uwezeshaji zilizofanyika hapo Wizara ya Kazi Uwezeshaji Wananchi kiuchumi na Ushirika Mwanakwerekwe.
Balozi Seif alisema mipango imara inaendelea kuimarishwa ya uwekezaji kwa kupatiwa fursa tofauti za kujiletea Maendeleo yao ya Kiuchumi na Kijamii.
Alizipongeza Saccos za Uwazi na Ushikavi kwa hatua yao ya kuungana pamoja na kuwa na Saccos kubwa ya Uwezeshaji Saccos ambayo itawaweka pamoja wafanyakazi hao kama suluhisho la kujiondolea matatizo.
‘‘ Naelewa kuwa Saccos ni suala la hiyari na sio la lazima. Hivyo na imani kwamba Saccos hii itakuwa mfano wakujifundishia nengine ’’.
Alisema Balozi Seif.
Aliitaka Wizara ya Kazi Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika ambayo ndio Mshirika Mkuu wa Wajasiriamali na Wananchi kuhakikisha ahadi inazotoa itazitekeleza ili kutoa Tamaa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliahidi kutoa Shilingi Laki 500,000/- kwa Vijana wa Kikundi cha Sarakasi cha Talent Group cha Mwanakwerekwe ili kujiimarisha Kiajira hapo baadaye
Pia ameahidi kumzawadia Bibi Mwandiwe Ali Makame wa Wilaya ya Kaskazini A aliyeshinda Shindano la Mama Shujaa Tanzania.
Balozi Seif amelikubali ombi la Wajasiri amali hao la kufanya Biashara zao kwenye kiwanja cha kisonge Jumba nambari mbili la Michenzani kila Jumapili na kusema atakuwa tayari kuwa Mgeni Rasmi katika Ufunguzi wa Soko hilo.
Aliuagiza uongozi wa Serikali wa Mkoa Mjini Maharibi kwa kushirikiana pamoja na Baraza la Manispaa kuandaa taratibu zitakazowezesha kuanza kwa soko hilo ikizingatiwa zaidi usafi wa Mazingira.
Naye Waziri wa Kazi, Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na UshiriKA Mh. Haroun Ali Suleiman alisema changamoto kubwa iliyopo hivi sasa ni kupambana na Umaskini ambalo limo ndani ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010.
Waziri Haroun alisema hilo litafanikiwa endapo nafasi za ajira zitaongezeka zaidi hasa katiika sekta ya uwezeshaji ambayo inachukuwa eneo kubwa la Vijana na Wanawake.
Akitoa Taarifa ya Wizara ya Kazi uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika, Katibu Mkuuwa Wizara hiyo Bibi Asha Abdulla alisema lengo la kuwa na Wiki ya Uwezeshji hapa nchini ni kutoa fursa ya kutafakari changamoto ziliopo.
Bibi Asha alisema Maadhimisho hayo ambayo ni kwanza kuanza kufanyika hapa Zanzibar yamekuwa na mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na makongamano, Bonaza la Machezo pamoja na Maonyesho ya Wajasiriamali.
Katika Maadhimisho hayo Balozi Seif pia alizindua Jengo la Ushirika wa Saccos ya Uwezeshaji ambayo tayari imeshakuwa na mtaji wa shilingi 40,000,000/- zinazozunguuka kwenye mfuko wao.
Uzinduzi huo umeenda sambaba na utolewaji vyeti kwa watendaji bora pamoja na hati za usajili wa Saccos hiyo.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

0 comments:

 
Top