Mamlaka ya Mitaji na Mendeleo ya Jamii ya wa Michigan Nchini Marekani imekubali kuisaidiA Zanzibar katika masuala ya Elimu, Afya na Mazingira.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Bwana Robert Shumake ametoa kauli hiyo wakati wa mazungumao yake na makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi mwishoni mwa ziara yake Nchini Marekani.
Bw. Shumake ambaye tayari ameshakutana na Uongozi wa Benki ya Watu wa Zanzibar PBZ ambao umenambatana na Balozi Seif katika ziata hiyo mamlaka hiyo inajitayarisha kuongeza misaada yake kwa Tanzania ikiwemo Zanzibar.
“ Tumeshatoa misaada ya vifaa vya elimu kwa Nchi za Bara la Afrika ikiwemo Ethiopia na Tanzania katika skuli za Mkoa wa Kilimanjaro” Alisema Bwana Shumake.
Alisisitiza kuwa Mamlaka yake imekuwa ikitoa fursa za kudhamini masomo ya elimu ya juu kwa wanafunzi wa Afrika wenye mazingira magumu.
Bwana Shumake alisema utafiti uliofanywa na Mamlaka yake umegundua watoto wengi wa Bara la afrika wanashindwa kuendelea na Masomo ya juu kutokana na kukabilkiwa na umaskini uliokithiri.
Alimueleza Balozi Seif kwamba bado wanaangalia uwezekano wa kutoa huduma katika sekta za Kilimo ikilenga zaidi vijana ambao kundi kubwa linakosa ajira na kujikimu kimaisha.
Naye Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif ameipongeza Mamlaka hiyo kwa uwamuzi wake wa kusaidia huduma za kijamii.
Balozi Seif alisema Familia nyingi hasa za kiafrika zimekuwa zinakosa huduma za kijamii na kukumbwa na maradhi.
Balozi Seif na Ujumbe wake unaondoka Marekani na unatarajiwa kuwasili nchini jioni ya Jumatatu ya tarehe 8/11/2011.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

0 comments:

 
Top