TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema mchango wa Jamuhuri ya Cuba katika kusaidia ustawishaji wa Afya za Wananchi utaendelea kuheshimiwa na kila mwana Jamii.
Balozi Seif ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Balozi wa Jamuhuri ya Cuba Nchini Tanzania Bw. Ernesto Gomez Diaz hapo katika Ofisi yake iliyopo katika Jengo la Baraza la Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Amesema Wananchi wa Zanzibar wameshuhudia juhudi zinazochukuliwa na Cuba katika kusaidia huduma za afya pamoja na utoaji mafunzo katika Sekta hiyo.
Balozi Seif amesema mfumo wa mafunzo ya afya unaotolewa na Wataalamu wa Afya wa Cuba umeongeza wigo wa upatikanaji wa huduma hiyo kwa urahisi.
“ Mfumo wa mafunzo ya Wataalamu wa Cuba kwa watendaji wa Afya wa Zanzibar umesaidia kupunguza uhaba wa Madaktari ambao wengi kati yao hubakia nje ya Nchi baada ya kumaliza mafunzo yao ”.
Alisema Balozi Seif.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif ameishauri Cuba Kuangalia uwezekano wa Kuwekeza Zanzibar katika nyanja ya Utalii.
Alisema Cuba tayari imeshapiga hatua kiasi katika sekta ya Utalii jambo ambalo linaweza kusaidia kunyanya kipato cha wananchi kwa kuongeza ajira hasa kwa Vijana .
Mpema Balozi wa Jamuhuri ya Cuba Nchini Tanzania Bwama Ernesto Gomez Diaz amesema Nchi yake inakusudia kuongeza mashirikiano na Mataifa ya rafiki katika kipindi kijacho. Bwana Gomez amesema mpango huo utazingatia zaidi Nchi za Bara la afrika.
Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameendelea kupokea mkono wa pole kutoka kwa taasisi kadhaa hapa nchini kusaidia mfuko wa Maafa Zanzibar
Akitoa mkono wa pole Mwenyekiti wa Jumuiya ya Ustawi wa Jamii Tanzania { TASO } Bw. Lenard Mbiliji amesema ufahamu wa Taaluma katika eneo la Ustawi wa Jamii bado halikidhi mahitaji yaliyopo.
Bw. Lenard amesema ipo haja ya uhamasishaji wa kuanzishwa kwa vyuo vya ustawi wa Jamii ili kuongeza idadi ya wahudumu.
Michango hiyo imekuja kufuatia Janga la kuzama kwa Meli ya M.V Spice Islanders tarehe kumi Septemba mwaka huu na kusababisha Maafa makubwa ya vifo pamja na kupotea kwa abiria na Mizigo kadhaa.

0 comments:

 
Top