TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Makampuni ya Bima Tanzania chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Bima Tanzania yamekubaliana kulipa fidia kwa madai yoyote yatakayowasilishwa kwa Makampuni hayo juu ya vifo, waathirika na majeruhi wa ajali ya M.V Spice Islanders iliyotokea Mwezi uliopita.
Mwenyekiti wa Bodi ya mamlaka ya Bima Tanzania Profesa Mgongo Kifimbo amesema hayo wakati akiwasilisha mchango wa Shilingi milioni 10,000,000/- kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo vuga Mjini Zanzibar kusaidia Mfuko wa Maafa Zanzibar.
Profesa Magongo amesema uwamuzi huo umefikiwa na Makampuni hayo baada ya kizingatia zaidi sababu za kibinaadamu , hivvyo kitachohitajika kwa wahusika hao ni kuwa na vielelezo kamili.
“ Wale waliofiwa watalazimika kuwa na uthibitisho wa vifo unaotolewa na mamlaka inayohusika wakati waathirika na walemavu watalazimika kuwa na vyeti vya daktari ”. Alisema Profesa Magongo.
Amesema kwa mujibu wa Sheria za Usafiri wa Baharini Meli yoyote iliyosajiliwa Zanzibar Lazima iwe na Bima. Profesa Mgongo alisema Meli ya M.V Spice ingawa haikuwahi kulipa Bima katika kipindi cha mwezi mmoja kabla ya kuzama kwake lakini bado Bima ya meli hiyo inaonekana kuwa na utata kidogo.
Hivyo Mwenyekiti huyo wa Mamlaka ya Bima Tanzania amesema Makampuni hayo yanahusika na ulipaji wa Bima hiyo huku taratibu za malipo hayo zikiangaliwa kwa kina.
Akipokea michango hiyo Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameendelea kuzishukuru Taasisi na Jumuiya Tofauti zinazochangia Mfuko huo kwa lengo la kuwafariji Wananchi waliokumbwa na Maafa ya kuzama kwa Meli ya M.V Spice Islanders mezi uliopita.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zaznaibar

0 comments:

 
Top