TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Watanzania wanapaswa kuendelea kuilinda hazina ya amani iliyopo nchini kwa lengo la kulinusuru Taifa kuingia katika mkumbo wa Machafuko yanayoweza kuleta maafa kwa kizazi kijacho. Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ametoa kauli hiyo hapo Afisini kwake Vuga Mjini Zanzibar wakati Akizungumza kwenye Kipindi Maalum cha Miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika kinachotayarishwa na Shirika la Utangazaji Tanzania { TBC }.
Balozi Seif amesema amani iliyopo Nchini imesaidia kupanuka kwa Demokrasia zaidi ndani ya Mfumo wa Vyama vyama vingi vya Siasa ulioanza tokea mwaka 1992. Amesema Jamii ya Watanzania imekuwa shuhuda ya machafuko ya kisiasa yaliyopelekea migogoro na maafa katika Baadhi ya Mataifa Duniani na hasa Nchi Jirani zinazoizunguuka.
“ Inafurahisha kuona Nchi inafaywa Uchaguzi kwa salama tafauti na Mataifa mengine Duniani na Hasa Barani Afrika ”. Alisema Balozi Seif.
Akizungumzia mfumo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ulioanzishwa hapa Zanzibar baada ya kupitishwa na Baraza la Wawakilishi mwaka 2010 Balozi Seif amesema mfumo huo umeleta faraja kwa Wananchi waliowengi Nchini. Balozi Seif amesema Serikali ya Umoja wa Kitaifa imekuwa Tiba ya kuondoa migogoro ya Kisiasa ndani ya Visiwa vya Zanzibar ambayo ilikuwepo Kabla ya Mapinduzi ya mwaka 1964 na baada ya kuanzishwa kwa mfumo wa Vyama vingi vya Kisiasa mwaka 1992.
“ Tunapaswa kujivunia masuala haya kwa vile utaratibu wa kutafuta suluhu na kufikia muwafaka huo hatukuhusisha Mataifa wala Taasisi za nje ya Nchi ”. Alisema Balozi Seif Ali Iddi.
Kuhusu wigo wa Maendeleo ya Demokrasia Nchini Tanzania Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema Wananchi tayari wamepata uwanja mpana zaidi wa kutanua Demokrasia. Amesema Demokrasia imefanya Maisha ya Wananchi kuwa ya harakati na kupelekea Kukuwa kwa haraka Maendeleo ya watu na hasa Vikundi pamoja na Taasisi za Kiraia.
Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa pia Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa Zanzibar ameendelea kupokea michango kutoka kwa wahisani mbali mbali kusaidia Mfuko wa Maafa.
Mchango aliopokea umetolewa na Jumuiya mbali mbali za Kidini zilizopo Mkoani Arushwa na kuwasilishwa na Bwana Gullam Hussein. Bwana Gullam amesema Wananchi wa Arusha walikuwa wakifuatilia Taarifa za Maafa yaliyowapata Wenzao wa Zanzibar na Kupelekea kufanya maamuzi ya kusaidia Waliopatwa na Maafa hayokufuatia kuzama kwa Meli ya M.V Spice Islanders hivi karibuni.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Mkamu wa Pili wa Ris wa Zanzibar

0 comments:

 
Top