Marehemu Professor Abdulrahaman Mohamed Babu alikuwa mwanasiasa, mwanamapinduzi ambaye alikuwa ni mkubwa mkubwa na muhimu katika upwa wa Afrika ya mashariki, mwandishi, mchumi, na ujamaa kwake ulikuwa ni mfumo wa maisha yake.
Tunapowataja na kukumbuka wakongwe wa siasa na wapambanaji waliosimama kidete kuhakikisha kuwa wafrika tunajikomboa kutoka katika makucha ya ukoloni uwe mkongwe au ukoloni mambo leo,jina la marehem Abdulrahman Mohamed Babu (RIP)alitasahulika, ambaye kama angelikuwa hai leo tarehe 22 September ndio siku yake ya kuzaliwa. Historia inatuelezea kuwa mwanamapinduzi marehem Prof. A.M.Babu alizaliwa 22 Sept 1924
huko kisiwani Unguja,Zanzibar, na alifariki dunia 05.08.1996, marehem Prof. A.M.Babu anakumbukwa kwa mengi pamoja na kuwa engineer wa mapinduzi ya visiwani 1964 yalimfanya sultani akimbie na kusahau kiremba kitandani

0 comments:

 
Top