Ajali za barabari zimekuwa zikichukuwa uhai wa watu wengi nchini Tanzania na hasa mabasi yafanyayo safari za mikoani kwenda jijini Dar-es-salaam, ambapo kwa njia moja au nyengine ajali hizo husababishwa na uzembe wa madereva au wamiliki wa mabasi hayo yatokayo mikoni
Hakuja haja ya kukumbuka mabasi kama vile Championi, Muhammed Trans na mengineyo ambayo yameweza kuchukuwa roho za abiri wake, huku baadhi ya wasafiri hao wakiwa wamebakia kuwa ni walemavu wa kudumu katika maisha yao yote
Wakati machungu ya ajali hizi za mara kwa mara zikiwa zinaendelea huku kikiwa na udhibit madogo wa kupunguza ajali hizo, kampuni yenye kumilika basi la Luck Star, limeamuwa kuwasafirisha abiria wake watokao Mwanza kwa muda wa masaa 24, kutoka saa kumi na mbili asubuhi ya terehe pili (2) hadi tarehe tatu 3-9-2011), hii ni kutokana na uzembe wa makusudi wakutokufanyiwa matengezo kwa wakati (service) bai lake lenye namba za usajili T 138 BDQ linafanya safari zake kutoka Mwanza- Dar karibu kila siku.
Kwa kuwa mmiliki wa gari hii bado ameshikili msimamo wa hesabu yake ya 1+1=11 badala ya 1+1=2, hali ambayo ilipelekea kutoa basi Mwanza na kulipeleka tupu bila ya abiri hadi kwenye basi liloloharibika lenye namba T 138 BDQ katika eneo la KIZAGA, wilaya ya Iramba Magharibi Singida.
Siwezi kusema kama mmliki wa kampuni ya Lucky Star Bus si mfanya biashara, lakini kutokana na hali halisi ndivyo inavyoonekama kama hana uwezo wa kuendesha biashara ya usafirishaji wa abiria kutoka Mwanza, Dar-es-salaam au hata maeneo mengine, kwani hakukuwa na haja ya kutoa basi Mwanza hadi Singida wakati basi lilopoharibika ni kilometa chache tu kufika Singida, kitu ambacho angeweza kufanya ni kumruhusu Dereva wake kuwapakia abiria wake kwenye basi la kampuni nyengine ili kuwawahisha safari yao
Inasikitisha kuona tajiri amethamini sana pesa na gari lake kuliko abiria ambao kwa njia moja au nyengine ndio wanaomuweka mjini na aonekane mzuri na mwenye kupendeza zaidi
Si hivyo tu, bali ukosefu wa kufikiria umuhimu wa abiria ameshindwa hata kuoneshsa ungwana na ikhsani kwa abiria wake ambao wameweza kumstahamilia kwa muda wote wa masaa 24 ya safari ya kutoka Mwanza-Dar, lakini kabla ya kupiga Dar basi hilo liliweza kutia nanga gairo, ambapo abiri walijipatia chakula, ambacho gharama zilipaswa kulipwa na kamapuni ya lucky star bus, lakini kinyume chake abiri walilazika kijilipia wenyewe na wakati watendaji wa kampuni hiyo wanaulizwa maswala juu ya kupeba ghara hizo walijibu kwamba wao hawana la kusema kwa vile kampuni haikutoa maelezo hayo.
“ kwa kweli mimi ninachojuwa ni kwamba gari ipo njiani inakuja na kuhusu masuala ya kuwapatia vymba vya kulala hilo haliwezekani kwani mnatakiwa nyote mtalala kwenye gari na wala hatuna utaratibu wa eti kuwanunulia chakula hilo lipo nje ya uwezo wetu” alisema mfanyakazi mmoja wa basi hilo alaitambulika kwa jina la Said
Nathubutu kusema kwamba inaonekana kwamba mpaka sasa hakuna sheria nadhubuti zinazohusiana na suala la usafirishaji wa abiria pamoja na usalama wa barabarani, ambazo zinampa fursa abiria kuweza kudai au kupewa fidia kutokana na uzembe unaosababishwa na kampuni ya basi husika.
Ipo haja kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri na hasa wa barabari kuweza kufuta taratibu na sheria za usafirishaji wa abiria ikiwa ni pamoja na kuwafikisha abria wao kwa wakati, na ikibidi iuchelewa basi ni wajibu wa mmiliki wa basi au kampuni hiyo ya usfirishaji kulipa gharama za malazi pamoja na chakula kama vile wamiliki wa usafiri wa anga wanavyofanya.
Si hivyo tu, ila pia ipo haja ya wamiliki hao kuweza kushirikiana na jeshi la polisi katika kuhakisha kwamba usalama wa abiri na mizigo yao upo, kama vile si vibaya ndani ya basi na hasa yale yanatembea muda wa usiku kuwa askaria angalau wamili, katika magari yao.
Najuwa inaweze ikaonekan ni vigumu kutekelezeka hili, kwa sababu wananchi walio wengi nchini Tanzania wanaishi kwa mazoweya zaidi kuliko uhalisia wa maisha yao, kwa mfano kuna sababu gani mmiliki wa gari ya abiri kuandika kwenye tiketi yake abiri “chunga mzigo wako” au “mzigo ndani ya basi si dhamana yetu” na mengine mengi
Sababu ya msingi ni kwamba mmiliki hayupo kwa ajili ya kumsaidia abiria bali yupo kwa ajili ya kumnyonyo na kumdhulumu abiria haki yake, kama vile bima, hii ni haki ya msingi kuipata kwa kila abiria asafiriye kwenye basi, daladala, tax nk. Lakini je haki hii abiria huipata kikamilifu au?
Utagundua kwama hakuna abiri yoyote Tanzania anayesafiri kwa basi au usafiri mwengine ambaye pindi akipata ajali hufaidika kutokana na bima ya chomba hicho, lakini mbali ya yote mmiliki anaendelea kuwa bepari huku akijuwa kwamba anavunja sheria, hali hii hadi lini?
Kwa sasa muda umefika mmiliki wa basi awe binadamu kamili badala ya kuwa ninyume chake.

0 comments:

 
Top