Hii ndio boti ya Ms Spice Islande ambayo imezama tarehe 11.09.2011 katika bahari ya Nugwi, na hii ni  boti ya pili ambayo imegharimu maisha ya watu wengi katika historia ya visiwa vya Zanzibar, ingawaje inasemekana kwamba zaidi ya watu mia mbili (200) wamefariki dunia kutokana na ajali hii. Hata hivyo watu waliookolewa na kuwa hai ni mia sita kumi na mbili (612) kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na mamlaka husika na bado inakisawa kwamba wapo baadi ya abiria inasemekana wamebakia ndani ya boti hii, mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi ameni

0 comments:

 
Top