kwa mara ya kwanza nchini Tanzania wameweza kuadhimisha siku ya haki ya kujuwa nchini kote.
Maadhimisho hayo ambayo ni ya kwanza tangu kuasisiwa kwake katika mji wa SOFIA nchini BULGARIA, kwa hapa Zanzibar shughuli hizo ziliendeshwa chini ya usimamizi wa Baraza la Habari Tanzania
Akifungua kongamano la maadhimisho hayo, Makamo wa Rais wa Baraza la Habari Tanzania, Nd.Chande Omar Chande, lengo kubwa la maadhimisho hayo ni kumuwezesha mwanachi kuweza kupata habari (kujuwa taarifa) na matoke mbali mbali yanayotokea ndani ya jamii yake
Makamo wa Rais alifahamisha kwamba kwa ujumla yapo mambo yasiyopungua manane ambayo ni ya lazima kwa kila binadamu kuweza kuyajuwa ambayo ni :-
  • Kupata habari ni haki ya kila mtu
  • Haki ya habari iwe kwa mujibu wa sheria
  • Haki ya habari ni ya kila mtu katika jamii
  • Kuomba kupata habari kusiwe na vikwazo
  • Watendaji wa serikali wawasaidie wanaotaka habari
  • kushindwa kutoa habari kuwajibishe muhusika
  • Taasisi za ummah ni lazima zitoe habari muhimu kwa jamii
  • Haki ya kupta habari ni lazima ilindwe na chombo huru
Tangu kuasisiwa kwa uhuru wa kupata habari dunia hapa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla ni mara ya kwanza kwa kufanyika kwa maadhimisho hayo

0 comments:

 
Top