Unaweza ukasema ni vinyonyo(danganya) kama ambavyo waswahili wengi wamezoweya kuita, lakini ukweli kwamba hizo zote ni rangi tu ila jina halisi ni kondomu ( mipira ya kiume) ambayo jamii imekuwa ikitumia kwa ajili ya kukidhi mahitaji yao ya kimwili. Ingawaje watu wengi wamekuwa wakidhani kwamba kondomu ni kinga halisi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi.
kitu cha msingi ni kujiuliza kama kweli kondomu zinasaidia kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa nini ukimwi unaongezeka kwa kasi kubwa nchini, huku kondomu zikiwa zimepewa majina na hadhi tofauti kulingana  na mahitaji ya mtumiaji mwenyewe.kitu kingine ni jambo la msingi kama mtu ataweza kufikiria kwamba kondumu ipo kwa ajili ya uzazi wa mpango tu na sio kwa ajili ya kupunguza maambukizi ya ukimwi .

0 comments:

 
Top