Imeelezwa kwamba ushirikiano katika ya jumuiya na jumuiya ni jambo la msingi katika kuendeleza uhifadhi wa mji mkongwe wa Zanzibar pamoja na maeneo mengine ya historia yaliyomo ndani ya Zanzibar
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Hifadhi ya Mji Mkongwe Nd. Mughery wakati alipokutana na Mkurugenzi wa Mkumbusho Bi Amina Ameri kwenye afisi za makubusho katika People Palace
Aidha Mwenyekiti Mughery alifahamisha kwamba jumuiya yake imekuwa ikifanya kazi kwa karibu sana na taasisi za kiserikali na hasa idara ya Makumbusho na Mamlaka ya uhifadhi wa mji mkongwe Zanzibar
Akizungumzia hali mbaya inayoyakabili magofu na badhi ya majengo ya mji mkongwe Mkurugenzi Amina alisema kwamba kwa sasa yapo matatizo madogo madogo ambayo yanatakiwa kufanyia kazi kwa ajili ya kuweza kuyaendeleza magofu na ambayo yamo ndani ya mji na nje ya mji wa Zanzibar pamoja na kisiwa cha Pemba

0 comments:

 
Top