Nyeupe au Nyeusi (WHITE & BLACK) ni makala (filamu )ya dakika 58, ilichukuwa ujumbe kuhusiana na unyanyasaji na mauwaji wanaopatiwa watu wanye athari za ngozi (ulemavu wa ngozi/albino) ambapo wao ni miongoni mwa jamii hii ya Kitanzania kwa mujibu wa sheriaz za nchini.
Katika Afrika mashariki, jumla watu wenye athari ya ngozi ni mara kumi zaidi kuliko ilivyo kwa watu wengine na hawa mwenye athari hii ya ngozi ambao  wanaopatikana katika mabara mengine kama vile Amerika ya kaskazini, Ulaya Asia n.k.
Inasadikiwa kwamba Barani Afrika kila mtu mmoja kati ya watu 2000 basi mtu mwenye atahri hii ya ngozi  (ulemavu wa ngozi) ni lazima atakuwepo.
Nchini Tanzania na sehemu nyingine za Afrika Mashariki baadhi ya waganga wa jadi ambao si wakweli wamekuwa mstari wa mbele katika kupoteza uhai wa watu wenye athari ya ngozi kwa kutumia viungo vya watu wenye ulemavu wa ngozi katika tiba zao, wakiamini kuwa viungo vya watu wenye ulemavu wa ngozi huleta bahati na mafanikio.
Makala hii ni zao la utafiti uliofanywa na Vicky Ntetema, Mwanahabari ambaye ameweza kuitumia vyema taluma yake ya habari na hasa katika suala zima la Investigative Journalism kwa kweli anahitaji pongezi za dhati kwa kuweza kufanikisha kazi hii ambayo kwa kweli ilikuwa ni hatari na yenye kuhatarisha maisha yake, kwa kiasi kikubwa utafiti wa Vick ambaye alizunguka nchi nzima akifanya utafiti juu ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi.
Utafiti wake ndio uleozaa filamu hii ya Neupe au Nyeusi ambapo pia imeweza kutuonesha hali tofauti ikiwemo iamni pamoja na wale wote ambao kwa njia moja au nyengine wamekuwa waathrika wa mauwaji haya ya kinyama katika taifa hili.
Makala hii imechaguliwa kuingia kwenye Tuzo ya Osmane Sembene, Tuzo ya Filamu inayohusisha Filamu zenye ujumbe wa kimaendeleo, itolewayo na Tamasha la Filamu za Majahazi Zanzibar.

0 comments:

 
Top