kwa mwanadamu kufa ni jambo la kawaida kutoka na mktaba aliofunga na mola wake tangu siku aliyokubali yeye kuja kusihi duniani
lakini kitu kibaya zaidi ni pale mtu au taifa moja kuwa na uwezo wa kuidangaya duniani kwa nyakati tofauti, sipingani na kauli za vyomba vya habari lakini hivi ni kweli mtu anaza kufa zaidi ya mara moja? hii ni miujiza au niudanganyifu tosha kutoka kwa wale wanaojiita wasomo na wababe wa dunia, haiwezekani hata kidogo binaadamu mmoja kufa mara tatu, kama ni hivyo tuambiwe inakuwaje hadi anafufuka kutoka kaburini na iuendelea kuishi?
kwa mfano mara ya kwanza karibu dunia kote ilitangazwa Osama bin Laden amefariki mwaka 2000, kama hiyo haikutosha mwaka 2005 tukatangaziwa tena na sasa mwaka huu wa 2011 pia amefariki tena katika mazingira yale yale ya mashambulizi ya makombora ya NATO
kibaya zaidi huku ni kutaka kumfananisha na Yesu ambaye atafufuka kutoka kwenye wafu siku ikifika, jee hii inaingia akilini au ni usanii tu wa kiahabari na kutaka sifa ambazo hazina ukweli? kwa hakika tunapswa kufahamu mtu mwenye akili timamu unaweza ukafanywa mpumbavu kwa wakati mmoja na si kwa wakati wote kama ambavyo hizi taarifa zinazodai kufa kwa kiongozi wa Al qaida Osama bin Laden
sote tunafahamu kwamba vita ni ujanja lakini siyo kwa aina hii ya kuidanganya dunia

0 comments:

 
Top