Ama katika vitu muhimu kwa binadamu mbali ya kula, kulala, maji safi, elimu nk, lakini pia suala la afya bora ni kitu muhimu kwa kila mwanadamu mwenye akili timamu
Ingawaje sula hili mara nyingi kwa wakazi wa ndani ya mji huwa wanawasukumia BARAZA LA MJI(MANISPAA) kama kwamba wao ndio wenye wajibu wa kutunza miji na fukwe za bahari
Kama tujuavyo visiwa vya Zanzibar kwa asilimia mia moja vimezungukwa na maji ya bahari kwa hivyo ni wajibu wa kila mwananchi(mwanakijiji) kutunza na kuhifadhi nmazingira kama ambavyo Jumuiya ya Uhifadhi ya Mji Mkongwe, ambavyo kwa kushirikia na taasisi mbali mbali nchini walikusanyika na kufanya usafi katika maeneo mbali mabali ya fukwe kama vile pwani ya Kizingo, Forodhani, Shangani n.k
Ingawaje hili oimefanywa na jumuiya isiyo ya kiserikali lakini je kwa watu wanaishi karibu na fukwe hizo ni nani anapaswa kuzilinda? na hasa tukiangalie zile sehemu ambazo kwa kiasi kikubwa fukwe zake zimekuwa kivutio kwa biashara ya utalii, kuna hatari kubwa ya uchafuzi wa mazingira ya bahari
Kwa hakika usafi ni tabia ya mtu, lakini pia usafi ni nidhamu bora kwa kila kiembe kwani hakuna kiembe yoyote yule ambaye anapenda kuwa mchafu vyenginevyo atakuwa na upungufu wa akili, ni haki na niwajibu kwa kila mtu kudumisha usafi katika maeneo yake

0 comments:

 
Top