Miraa (Mirungi au Gomba) ni miongoni mwa biashara maarufu nchini kenya na kwa kweli ni biashara ambao hufanyika bila ya kificho wala aibu yoyote.
Ingawaje Miraa, ama Mirungi ama Gomba kwa kawaida huwa haina tofauti yoyote na kilevi kama vile BANGI au MADAWA mengine ya kulevya kama vile COCANE nk
Ingawaje ni kitu kinachopendwa na kila mtu kutoka katika rika mbali mbali, lakini athari zake kiafy ni kubwa na ni mbaya kwa wanando kwani mara nyingi huwa inapunguza hafu ya kuweza kumfariji wenzio ukiwa nyumbani hapa ninamaana kwamba watumia wengi wa miraa au mirungi kwa asilimia kubwa huwa hawana hammu ya kufanya mapenzi na wake zao
Hii ni kwa sababu watumia wengi ambao nusu na robu ni wanaume kwa kiasi kikubwa nguvu za kiume hupungua kwa kiasi kikubwa ingawaje mtumiaji mwenyewe huwa hakubaliani na hilo lakini hii ni kawada kwa mtu yeyote ambaye anatumia madawa ya kulevyo 
Unaweza ukakubalina na hilo baada ya kupata ushari wa kitabibu lakini ni muhimu kufahamu kuwa kwa mtu ambaye anatumia miraa ni lazima avute sigara na hiyo sigara peke yake inakemikali zisizo pungua elf nne(4000)  na ndio maana wanawake wengi ambao waume zao ni watumiaji wa miraa ni rahisi mno kwenda nje ya ndoa(kufanya mapenzi ) kwa ajili ya kutafu mtu wa kumfariji hii.
Kwa kweli hii ni hatari, ingawaje nchi kama Tanzania ukikamatwa na Miraa au Mirungi hii ni kesi na ikithibitika unawez ukatumikia kifungo cha miaka kuni na tano au zaidi kutegema na uzito wa kezi yenyewe lakini kwa wenzetu Kenya hili kwao si tatizo na ndio maana kila pembe utayopita muda wa jioni(magharibu) utavikuta vikundi vya Wasomali na hata wenyeji wa Mombasa wakiwa wanatafuna mirungi bila ya wasi wasi wowote, ni vyema kujifikiria mwenye kwa ubora na usala wa afya yako. kwani kinga ni bora kuliko tiba

0 comments:

 
Top