Arterial Network Tanzania imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya ajali iliyotokea Usiku wa tarehe 21/02/2011 katika barabara kuu ya Iringa-Morogoro kwenye eneo la Hifadhi ya Wanyama ya Mikumi na kusababisha vifo vya watu 13 wakiwemo wasanii wa Kundi la Muziki la Five Stars Modern Taarab na wengine kadhaa kujeruhiwa. Wasanii hao walikuwa wakirejea Dar es Salaam kutoka Mbeya ambako walikuwa wamefanya maonyesho.
Aidha Arterial Network Tanzania inaungana na familia za wafiwa na wasanii wote nchini kwa maombolezo ya msiba huu mkubwa katika sekta ya sanaa na taifa. Mwenyezi Mungu azilaze mahali pema peponi roho za Marehemu amen
Hata hivyo, Arterial Network Tanzania inawapa pole na kuwata majeruhi waliosalimika katika ajali hiyo wawe na moyo wa subra na kuwaombea dua kwa Mwenyezi Mungu wale wote waliotagulia mbele ya haki na kuwaombea wale wote walipata majeraha wapone haraka ili hatimaye waweze kurudi katika hali yao ya awali na kushiriki shughuli za sanaa.
Hassan Bumbuli
KATIBU
ARTERIAL NETWORK TANZANIA

0 comments:

 
Top