Kinadharia kila mtu ni mwandishi lakini inapaswa tufahamu kwa kunatofauti kubwa katika ya mwandishi na mwandishi wa habari, kwani MWANDISHI WA HABARI ni mtu ambaye amepatiewa elimu na njia maalumu za utafutaji, ukusanyaji pamoja na usambazaji wa habari zenyewe iwe kwa kupitia Radio, Tv, Magazeti, Online Journalism n.k
Lengo langu kuu ni kutaka kuonesha kwamba kwa hivi sasa nchini Tanzania pamoja na Visiwa vyake vya Zanzibar kumekuwapo na wimbi kubwa la kila mtu asiyekuwa na kazi ya kufanya hujiita mwandishi wa habari, lakini ukimwambia wapi amesomea taaluama hiyo, au akuoneshe cheti chake huwa hakuna jibu sahihi na ndio waana uvunjifu na mmongonyoko mkubwa wa maadili katika fani hii unaonekana kukuwa kwa kiasi kikubwa.
Na ndio maandio maana nikasema kwamba wao hao ni waandishi tu kwa vile walipitia darasani kwa ajili ya kuwaju kusoma na kuandika kwa maana hiyo hawi sawa na hafanani hata kidogo na Mwandishi wa habari.
Ipo haja kwa wamiliki wa vyombo vya habari, wahariri kubadilika kuchukuwa watu ambao inawezekan kwa njia moja au nyengine akawa nirafiki, mpenzi wake au ndugu yake wa damu, lakini jee kazi hii inakwenda katika misingi hiyo?
Ni vyema kufahamu kwa jamii yoyote ile ambayo haina maadili ni sawa na kundi la wanyama pori

0 comments:

 
Top