Zanzibar International Film Festival (ZIFF) inapenda kuwataarifu kuwepo kwa ZIFF Mini-Festival itakayofanyika Ngome Kongwe, Zanzibar kuanzia tarehe 31/12/2010 hadi 2/01/2011, itakua ni Tamasha dogo la siku 3 katika kutoa muamko kwa Tamasha kubwa la ZIFF lijalo (2-10 Julai, 2011).
Tamasha hili dogo litajumuisha filamu za kitanzania peke yake (Bongo Films) ili kuendelea kutoa mwamko kwa watengenezaji filamu wa Tanzania kufanya vyema katika tasnia hii, Tamasha hili litaonesha filamu 6 za Kitanzania na filamu 2 bora kati ya hizo zitaenda kuoneshwa katika Tamasha kubwa la filamu Afrika - FESPACO huko Burkina Faso.
Kama ilivyo ada ya Tamasha la Filamu la Nchi za Majahazi, tutakua pia na makundi ya muziki na wakati huu kundi zima la THT litafanya maonesho kwa siku zote tatu, watakao kuwepo ni Mwasiti, Marlaw, Mataluma, Amin, Barnaba, Pipi, THT Dancers na wengineo. Kwa habari zaidi tembelea www.ziff.or.tz
Tamasha la ZIFF limekuwa na mafanikio makubwa kimataifa mwaka huu. Tarehe 3-5 Decemba ZIFF ilionyesha filamu zake huko Potsdam Ujerumani ambako mtengenezaji filamu Sajani Srivastava alionyesha filamu ya Bongo "Nani" ambayo iliwafurahisha sana watazamaji.ZIFF pia ilionyesha filamu zake katika tamasha la Trinidad and Tobago na pia inatarajia kuonyesha filamu zake huko New york African Art Museum mwaka ujao.Tayari matayarisho ya Tamasha la 14 yameanza na kwa sasa kuna uhakika wa kuwa na Workshop juu ya utengenezaji filamu itakao endeshwa na Deustsche Welle ya ujerumani. Kwa upande wa Muziki Couds Entertainment wameingia mkataba na ZIFF kuendesha shughuli za muziki katika ZIFF. Magwiji hao wa Muziki wanatarajia kuleta mastaa wa kimataifa pamoja na kuwanadi zaidi wanamuziki wa Kitanzania.

0 comments:

 
Top