takaribani mi miezi mitatu au minne iliyopita wakaazi wa kisiwa cha Unguja walikuwa katika kiza totoro, lakini kwa sasa afadhali kwani umeme umerudi na shughuli zinaendela kama kawaida
ingawaje umeme umerudi, lakini bado kuna tatizo kubwa la ukosefu wa maji safi na salama kwa watumia wa kisiwa hicho
ijapokuwa ukisema kusekana kwa maji safi na salama ni tatizo, lakini jamii au mamlaka husika inaweza ikakuuliza jee kuna watu wangapi walipata kipindupindu kwa kipindi hiki? jibu hakuna lakini jee tunasubiri hilo litokee au?
ikiwa umeme tulichukuwa muda kustahamili kwa sababu muhimu ambayo kila mtu alikuwa anajuwa, leo hii kwa nini Mamlaka ya maji Zanzibar inashindwa kutoa taarifa rasmi juu ya tatizo la maji?
si dhani kama kukaa kwao kimya kunaweza kukamfanya mtu wa kawaida kuamini kwamba kunatatizo bali itaonekana kama vile wamedharau tu na si vyenginevyo
kwa kweli ifike muda jamii ibadili tabia na hata Mamlaka nayo inatakiwa kubadilika kwa vile ni chombo kilichopewa dhamana na kuheshimiwa na jamii kama imeshindwa si vibaya nafasi hiyo wakamkabidhi mtu mwengie awezaye kushughulikia suala la maji visiwani hapa

0 comments:

 
Top