Abdulrazak Gurnah amezaliwa mwaka 1948 katika visiwa vya Zanzibar ambavyo vipi katika mwambao wa bahari ya Afrika ya Mashariki.

kutokana na maelezo tuliyoyapata kutoka katika chanzo cha habari na pia kutoka kwenye web site www.contemporarywriters.com, Ab dulrazak Gurnah aliingia nchini Uingereza kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 1968 kama mwanafunzi na sasa ni Mwalimu ambaye anafundisha katika chuo kikuu cha Kent (University of Kent) nchini humo.
Aidha Gurnah ni miongoni mwa wahariri katika jarida lijulikananalo kwa jina la WASAFIRI (journal Wasafiri).Hata hivyo, Abdulrazak ni mtunzi ambaye kwa sasa amefanikisha kutunga vitabu vitatu, kitabu chake cha kwanza alikipa jina la Memory of Departure (1987), kitabu chake cha pili alikipa jina la Pilgrims Way (1988) na kila cha tatu ambachi kilipewa jina na la Dottie kilichapishwa mwaka (1990). Katika machapisho haya yote kwake Abdulrazak ni kitu amabcho kiweza kumpatia kumukumbu nzuri tangu kuhamia nchini Uingereza akitokea Zanzibar.

Ingawaje kitabu chake cha mwisho kilikuwa ni DOTTIE, lakini katika mwaka 1994 mtunzi huyu wa Kizanzibari aliweza kutoa kitabu kingine alichokiita kwa jina la Paradise, ambacho kwa kiasi kikubwa kimeweza kuelezea hali halisi ya wakoloni katika mwambao wa Afrika ya Mashariki kuanzia vita vya kwanza vya dunia n.k.

Mbali na hayo, katika kuendelza fani yake ya kutunga vitabu vyenye hadithi tofauti mnamo mwaka 1996 alitunga kitabu kingine kiitwacho Admiring Silence, ambacho kimeweza kueleza taarifa na halia halisi ya maisha ya vijana wa Kizanzibar ambao wamaehamia nchini Uingereza na baadhi yao wakiwa wameoa au kuolewa huko. Aidha Abdulrazak Gurnah aliweza kuitembelea baada ya miaka 20 ya kuishi Uingereza katika mwaka wa 2001.

0 comments:

 
Top