kwa kawaida funzo ni kitu muhimu kwa kila mwanataluma hapa nchini.

kwa siki hii ya pili ya mafunzo haya ya kutengeneza blog, kwa kweili nimeweza kujifunza mengi katika suala zima la blog na umuhimu kwa mwandishi wa habari hapa nchini.

ingawaje watu wengiwanadhani kwamba blog zipo kwa ajili ya kuonesha picha za nusu uchi au matukio meningine ya utadaku, lakini ukweli si hivyo kwani blog miongoni mwa njia moja wapo za kuwez kumpatia mtu habari za matukio tofauti yanayojiri nchini na hata sehemu nyengine duniani

kwa hakika MISA-TAN kwa kushirikiana na VIKES kutoka nchini Finland limeweza kuisaidia jamii ya wanahabari wengi nchini kwani limeweza kupita katika mikoa tofauti na hatime mafunzo hayo yametia nanga katika visiwa vya Zanzibar na kuweza kuwakutanisha Waandishi wa Habari kutoka Pemba na wale wa Unguja katika ukumbi mmoja wa chuo cha SUZA.

Kwa hakika kwa siku hii ya leo niweza kujifunza mengi mno ikiwa ni pamoja na kuzipitia na kuzikaguwa web site tofauti zikiwemo zile maarufu kama vile BBC,CNN, ALJAZEERA, VOA n.k

mbali na hayo, ili mafunzo ni vyema basi mwisho wa mafunzo hata Mwalimu Peik angeweza kutengeneza link moja na ile ya wale ambao waliapata mafunzo kule Tanzania bara

0 comments:

 
Top