kwa mujibu wa tafiti uliofanywa na wataalamu kutoka nchini Marekani wameeleza kwamba, Waafrika wanaougua ugonjwa wa malaria huenda wakawa wanapata matibabu ya kiwango cha chini kiasi ambacho inonekana kuwa ugonjwa huo kuwa ni sugu kwa sasa.
Watafiti hao kutoka kundi la Pharmacopeia, nchini Marekeani wamegundua kwamba asilimia 26 na 44 ya dawa za kutibu ugonjwa wa malaria katika nchi kama Uganda, Senegal na Madagasacr ni zenye uwezo mdogo wa kutibu ugonjwa huu.
Aidha, kundi hilo la wachuguzi, linafanya utafiti kwa niaba ya shirika la afya duniani WHO, limesema kuwa dawa za kutibu malaria zenye viwango vya chini hutumiwa kwa ajili ya matibabu ya ugonjwa huo, katika hospitali za umma pamoja na zile za binafsi.
Mbali na hayo,WHO imeonyesha wasiwasi juu ya matumizi ya dawa hizo, ambazo zinakisiwa kuwa na uwezo mdogo wa kutibu ugonjwa wa malaria.
habari hii imepatikana kutoka kwenye shirika la habari la BBC

0 comments:
Post a Comment