imekuwa ni jambo la kawaida kwa kila mtu, jambo lolote baya humvumishia mtoto ili yeye aweze kujisafisha na uovu alioufanya, mara utasikia huyu siku hizi hana adabu, wengine watoto wa siki hizi, sijuwi huyu mzee ana watoto wangapi katika visiwa hivi vya Zanzibar?
ingawaje kila kitu kibaya au makosa mengi huambiwa Mtoto kama chaka la uovu na ndio maana mara nyingi huambulia kipigo hata kama hana kosa la kupigwa ili mradi tu aadhibiwe
kwa hakika muda umefika kwa jamii na wanafamilia kwa ujumla kuweza kujiuliza ni njia ipi mwafaka kwa sasa katika kuwaadabisha watoto? ni kipigo, kumuonya kwa maneno au kumfahamisha njia iliyobora?
kama adhabu ya bakora ingekuwa ni tiba basi ingetosha kabisa kufanya jamii hii kuwa yenye nidhamu ya hali ya juu kabisa, lakini kwa kuwa kupiga au kumtusi mtoto sio dawa na ndioa maana wakazaliwa watoto wa siku hizi
ni wajibu wa kila mtu ( mzazi) kutafuta njia mbadala za kuweza kumuadhibu au kumfunza mtoto wake ,badala ya kumtukana au kumdhalilisha kwa maneno, au kumpiga mithili ya punda , jamii inapaswa kurudi katika mafunzo ya dini badala ya zile mila na dasturi za kidunia pekee ambazo kwa kiasi kikubwa hazina faida yoyote katika maisha yao, zaidi ni upotofu na dharau katika jamii zao
0 comments:
Post a Comment