Na,Jumbe Ismailly,Manyoni
KAYA 19 za Kijiji cha Sukamahela,tarafa ya Kilimatinde,wilayani Manyoni,Mkoani Singida zilizopo katika mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF awamu ya tatu zimemlalamikia afisa mtendaji wa Kijiji cha hicho,Ernesti Gyunda Kitundu kwa kile walichodai kuwa amewakata shilingi 2,000/= kwa kila kaya kwenye malipo yao.
Kwa mujibu wa wanufaika hao wa mpango wa kunusuru kaya maskini,kiasi hicho cha fedha walichokatwa kinagharamia malipo ya posho ya askari wa jeshi la mgambo aliyekwenda kuwapa taarifa za kwenda kupokea malipo yao ya mwezi julai na augusti,mwaka huu.
Wanakaya hao 19 walibainisha hayo wakati wa kupokea malipo yao waliyopewa taarifa za kwenda bila kukosa kuhudhuria kwenye ofisi za afisa mtendaji wa Kijiji hicho kupokea malipo ya mwezi Nov na Dis,mwaka huu.
Hata hivyo baada ya majina yao kutoonekana kwenye orodha ya majina ya walipwaji kwa mwezi huo wa nov na dis,hawakusita kuelekeza shutuma zao kwa afisa mtendaji huyo kuwa ndiye aliyechangia wao kutopata malipo yao ya mwezi nov na dis,mwaka huu.
Wanufaika hao kwa masikitiko makubwa walisema watendaji wa mfuko huo wamekuwa wakiwachezea sana bila wao kufahamu ni sababu au kigezo kipi kinachowafanya mara wawepo kwenye mpango huo wa kunusuru kaya maskini na wakati mwingine kujikuta majina yao hayapo kwenye orodha ya walipwaji.
Walifafanua kwamba mchezo huo ulianza wakati wa malipo ya mwezi julai,mwaka jana,ambapo licha ya kualikwa kuhudhuria siku hiyo kwa lengo la kupokea fedha hizo,lakini walipokwenda majina yao hayakuweza kuonekana kwenye orodha ya walipwaji,na walipohoji hapakuwa na majibu yanayoeleweka kutoka kwa watendaji kutoka wilayani.
Pamoja na malalamiko yao hayo,lakini hali hiyo iliendelea mpaka mwezi saba na wa nane mwaka huu ambapo walijulishwa tena kufika katika ofisi za mtendaji huyo wakati wa malipo ya muda huo na kukuta majina yao yapo katika orodha ya walipwaji hali iliyowafanya waondoke katika eneo hilo wakiwa na furaha isiyokuwa na kifani.
Lakini cha kushangaza hali hiyo ilijirudian tena katika malipo yaliyolipwa jumamosi ya nov,28 baada ya kutangaziwa kufika saa mbili asubuhi ambapo walikaa mpaka watendaji waliokuwa wamefuatana na wanakamati walipofika kati ya saa sita na saa saba mchana,kitendo kilichowafanya waridhike kwa kuamini malipo yao yatakuwepo.
“Hivi kweli mtakuwa mmetutendea haki kwa kutotupatia malipo yetu kwani tangu tuanze kuwasubiri saa mbili asubuhi mpaka saa hizi saa kumi jioni halafu mnasema majina yetu hayopo kwenye orodha ya walipwaji,je ni halali hiyo?walihoji wanakaya hao
Kutokana na kutoridhishwa na tukio hilo ndipo wawakilishi hao wa kaya 19 waliamua kurudisha fomu walizokuwa wamekabidhiwa kwa ajili ya kupokelea malipo na kuwataka watendaji hao kutoendelea kuwatapeli na badala yake wasijulishwe chochote juu ya malipo hayo zaidi ya kuwaruhusu wao waendelee kupokea malipo hayo kama walivyoamua kuwatoa wao.
“Hivi ninyi mnatuonaje sisi tuliokaa hapa tangu asubuhi kuwasubiri halafu mnatuambia majina yetu hayapo ni sababu zipi zilizowafanya msitupatie taarifa hizo mara tu mlipofika ili tuondoke tukajitafutie riziki kwa njia zingine,maana tumeshinda na njaa na sasa tutakwenda kulala na njaa”walisisitiza huku wakielekeza shutuma zao kwa afisa mtendaji wa kijiji hicho.
Alipotakiwa kuzungumzia kuhusu malalamiko ya wananchi wa kijiji hicho kuhusu kuwakata shilingi 2,000/= kwa kila kaya,afisa mtendaji wa Kijiji cha Sukamahela,Ernest Gyunda Kitundu alikanusha kuwa kaya 19 zilikatwa fedha zao kwa ajili ya kumlipa mgambo na kwamba ni kaya tano tu ndizo waliomuahidi mgambo aliyewafuata kuwajulisha taarifa ya malipo hayo na wala siyo kaya zote.
Hata hivyo Kitundu alisisitiza kwamba baada ya malalamiko hayo amefuatilia na kuwabaini watu wote walioahidi kumpatia askari wa jeshi la mgambo kiasi hicho cha fedha na kwamba hata hivyo siyo watu wote waliolipa 2,000/-= kwani kuna baadhi yao walitoa shilingi 1,000/=tu.
Akizungumzia malalamiko ya wananchi waliokatwa fedha kwa ajili ya kumlipa mgambo,Mratibu wa TASAF wilaya ya Manyoni,Labani Sagali alisema hakuna sheria inayoruhusu wananchi kukatwa fedha kwenye malipo yao kumlipa mgambo,bali malipo ya mgambo yatatokana na fedha wanazopatiwa serikali ya kijiji.
“Mimi sina taarifa hizo lakini kuanzia sasa nitafuatilia na kwa kuanzia nitamjulisha afisa mtendaji huyo ili aweze kuwarudishia fedha zote wananchi waliochangia malipo ya gharama za mgambo”alifafanua Sagali
Kwa mujibu wa mratibu huyo katika kuondoa shaka kwa wananchi hao ataan daa mkutano wa hadhara kwa wananchi wa kijiji hicho na kumtaka mtendaji kurejesha kiasi cha fedha zote alizowakata wananchi mbele yao kwa lengo la kujenga imani kati ya wananchi na uongozi wa TASAF wilaya ya Manyoni.

0 comments:
Post a Comment