Chama Cha Wananchi CUF kimemtambulisha rasmi Mansoour Yussuf Himid kuwa mwanachama anayeweza kukiwakilisha chama hicho katika Jimbo la Kiembesamaki.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika viwanja vya bustani ya Kiembesamaki, Katibu Mkuu wa chama hicho Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amesema ameridhishwa na Mansour kutokana na ujasiri alionao katika kuwatetea wananchi.
Amesema Mansour ambaye alikuwa Mwakilishi wa jimbo la Kiembesamaki kupitia Chama Cha Mapinduzi ni mzalendo wa kweli anayeipenda nchi yake, na kuwaomba wananchi wa jimbo hilo kumuunga mkono.
Nae Mansour Yussuf Himid amewaambia wanachama wa CUF kuwa tayari ameshachukua na kurejesha fomu ya kugombea uwakilishi katika jimbo hilo kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Amewahimiza wazanzibari kuungana na kuendeleza umoja uliopo, ili kuona kuwa maridhiano yaliyoasisiwa hapa Zanzibar yanafanikiwa kwa maslahi na ustawi wa Zanzibar.
Hassan Hamad, OMKR
0 comments:
Post a Comment