Ni muda sasa tangu kampuni ya Airtel kuweza kufanya kazi zako kutoka kwenye mikono asili ya TTCL, hatime CELTEL na sasa AIRTEL.
Ingawaje matangazo yake ni mazuri lakini ni yenye kukirihisha sana endapo uatweza kuyafanyia utafiti wa kisarufi, kwa ufano ni hili tangazo lao la hivi karibuni lenye kusomeka HAKATWI MTU HAPA, suala ni kwamba kama mtu hakatwi nani anakatwa wakati mji, mnyama, ndege na hata wadudu hawatumi njii ya maswaliano ambayo mwanaadamu peeke kutokana na akili zake ndio mwenye kutumia mawasiliano ya simu hapa nchini.
Inasikitisha kuona Airtel imeajiri watu ambao ni watoa hudama kwenye namba 100 ambayo ni hudukwa wateja ( custome care/call center) lakini cha ajabu wengi wa wahudumu wao hujadili mambo yasio ya msingi wowote, kwa mfano tarehe 20 mwezi huu, mtumiaji mmoja ambaye yupo Zanzibar alipiga kwenye kituo hicho lakini wahudumu walikuwa wakizungumza masuala yao binafsi na ambao yapo nje na kituo cha kazi.
Ingawaje mtumia huyo wa Airtel hakuridhika ndipo alipojaribu kupiga tena simu kwa mara nyingine na kupokelewa na muhudumu mwengine, licha ya kwamba alisikilizwa lakini, kwa kuwaondoshwa njiani aliambiwa kunahuduma amejiunga na alishauriwa ajitowe, kitu ambacho inaonekana wahudumu hao hawakuwa makini na kazi zao.
Si wezi kusema kwamba bango la sasa la hakatwi mtu lipo sawa, kwani ni kuwadanganya Watanzani kwa kuwakata pesa zao kiholela na kukosa hudumua walioitaka na hasa balaa linakuja pale unapojiiunga na vifurushi vyao vya internet, ni dhahiri kwamba huu ni wizi na ipo haja kwa kampuni ya Airtel na wengine kuweza kuwa makini kwani huduma ya mawasiliano ni jambo muhimu kwenye taifa.
Airtel Tanzania inapaswa kufahamu kwamba upuuzi wao wa kuwaibia wananchi umeshawatosha na wanapaswa kubadilika kwani zipo kamapuni nyingi ambazo zinaweza kutoa huduma ikiwa wao wameshindwa na hii ni dalili ya wazi ya kuanza kufilisika . na kwa mfumo huu nathubutu kusema ni kweli kwamba Airtel yatosha na si mchezo.
0 comments:
Post a Comment